Tanzania visiwani Wakati mazungumzo ya kutatua mgogoro wa
kisiasa Zanzibar yakiendelea, utendaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK),
unaonekana kupar
aganyika baada ya mawaziri wa CUF kususia kazi, wakidai
Serikali hiyo imeshamaliza muda wake.
SUK ni matokeo ya maridhiano kati ya chama
tawala CCM na CUF na ilianza kufanya kazi mwaka 2010, lakini uamuzi huo wa
chama hicho kikuu cha upinzani unamaanisha kuwa SUK sasa inafanya kazi kwa
mawaziri kutoka upande mmoja tu.
Zanzibar, ambayo ilifanikiwa kumaliza mgogoro
wa kisiasa ulioibuka katika chaguzi za mwaka 2000 na 2005, iliingia tena kwenye
mgogoro Oktoba baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (ZEC), Jecha Salum Jecha
kufuta matokeo ya urais wa visiwa hivyo na ujumbe wa Baraza la Mawakilishi kwa
madai ya sheria na taratibu kutofuatwa, wajumbe wa ZEC kutofautiana na mmoja wa
wagombea kujitangaza mshindi na akaahidi kuitisha uchaguzi mwingine ndani ya
siku 90.
Kwa sasa imekuwa ikiripotiwa kuwa Rais wa
Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na Makamu wake wa Kwanza, Maalim Seif Sharif
Hamad ambao waliogombea urais wamekuwa wakiendelea na mazungumzo kuhusu suala
hilo lakini hayajawekwa bayana.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake kutoka CUF,
Said Ali Mbarouk alidai Serikali imewaingizia mishahara kinyemela, kitu
alichosema si halali.
Mbarouk, aliyekuwa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Utalii na Michezo, alisema wameshaandika barua Wizara ya Fedha ya
Zanzibar iwape namba ya akaunti ili wazirejeshe fedha hizo alizoziita batili.
Alisema hawakuona haja ya kumuandikia Rais
barua za kujiuzulu kwa kuwa muda wake umeshaisha kisheria. Hata hivyo, ukomo wa
Rais kwa mujibu wa Katiba, humalizika mara baada ya kuapishwa mgombea
aliyeshinda kwenye uchaguzi.
Wakati Mbarouk akisema hayo, Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alisema
pamoja na kwamba hawanyi kazi, mawaziri hao wanalipwa mishahara.
“Mimi hayo si mamlaka yangu kisheria ingawa
wanalipwa. Hawajakanusha, wala hawajaandika barua,” alisema Aboud. “Sisi tupo
kihalali kutokana na mambo mawili, tafsiri aliyoitoa Mwanasheria Mkuu (Said
Hassan Said) na pia kikatiba. Kimantiki, Serikali ipo na uhalali huo upo na
iwapo wao wanapinga, basi nasema waende mahakamani kupata ufafanuzi wa Katiba.
Lakini Aboud alisema uamuzi huo wa
unadhoofisha utendaji na kuathiri ufanisi wa SUK.
Post a Comment