0

1.Kassim Majaliwa anakuwa Waziri Mkuu wa Pili kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu baada ya Mizengo Pinda.
 
2.Hadi sasa ni waziri mkuu mmoja aliyeshika wadhifa huo akiwa serikali mbili tofauti, Rashid Mfaume Kawawa- Tanganyika na Jamhuri ya Muungano.
 
3.Ni Mzanzibari mmoja tu amewahi kushika wadhifa huo, Dk Salim Ahmed Salim.
 
4.Ni Waziri Mkuu mmoja tu aliyetumikia nafasi hiyo kwa miaka kumi, Frederick Sumaye (1995-2005)
 
5.Ni watu wawili tu waliotumikia nafasi hiyo kwa vipindi viwili tofauti, Edward Sokoine (1977-1980, 1983-1984) na Cleopa Msuya (1980-1983-1994-1995).
 
6.Ni Waziri Mkuu mmoja tu aliyekufa akiwa madarakani, Edward Sokoine (1984).
 
7.Ni Waziri Mkuu mmoja tu aliyejiuzulu kwa kashfa, Edward Lowassa (2008).
 
8.Ni mawaziri wakuu wawili waliojivua uanachama wa chama tawala, Edward Lowassa na Frederick Sumaye (kutoka CCM 2015)

9.Ni Mawaziri Wakuu wawili tu waliotokea vyama vya wafanyakazi, Julius Nyerere na Kassim Majaliwa.

Post a Comment

 
Top