0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli,asubuhi hii amemuapisha Mbunge wa Ruangwa, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania mjini Dodoma.

Hafla ya Kumuapisha Mh. Majaliwa imefanyika kwenye Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali wakiwemo, Makamu wa Rais wa Tanzania, Bi. samia Hassan Suluhu, Rais wa Zanziba, Dk. Ali Mohammed Shein, Makamu wa Rais Msitaafu, Dk. Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Job Ndugai na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, Wabunge, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange, Wabunge na wageni wengine.


Ni waziri mkuu aliyepita bungeni kwa asilimia 73.5 ya kura zilizopigwa na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
ikiwa Idadi ya wabunge ni 394 waliosajiliwa ni 369 na waliohudhuria Bunge ni 351


  • Aligiwa kura 258
  • Zilizoharibika ni kura 2
  • Kura za hapana 91






.

Makamo Wa Rais Mstaafu Awasili Hafla Ya Kumwapisha Mhe Majaliwa

or

Post a Comment

 
Top