Rais Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli leo wameongoza wananchi,Viongozi wa serikali ndugu na jamaa kumuga aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana kwa ajali ya Chopa mkoani Morogoro.
Marehemu Filikunjombe ameagwa leo nyumbani kwake Mtoni Kijichi jijini Dar es salaam ambapo mara baada ya kuagwa atasafirishwa kwa ndege kuelekea nyumbani kwake Ludewa kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho.
Historia ya Filikunjombe kwa ufupi,
1.Deo Filikunjombe kamaliza shahada yake ya Mass Communication Makerere University Uganda
2.Alikuwa Ripoter wa Radio One na ITV kwa muda mrefu akitumia jina la Deo Haule akiripoti toka Kampala.
3.Alijiunga na Jeshi la Polisi na kufanya kazi kwa mwaka mmoja kisha akaacha kazi sababu alipangiwa kitengo cha Habari makao makuu ya Polisi na kufanya kazi chini ya Mohamed Mhina.
4.Alipotoka Polisi alijiunga na World Vision kama Communication/ Information Officer na kufanya kazi kwa miaka kama minne hivi akiwa Makao makuu Arusha na baadae akahamishiwa tawi la Dar es salaam
5.Alipotoka World Vision akajiunga na MKURABITA ambapo alifanya kazi kwa muda usiozidi miaka miwili akaacha.
6.Baada ya kuacha Mkurabita, ndipo akaanza harakati za kuingia kwenye siasa na kuchaguliwa kuwa mbunge mwaka 2010.

Post a Comment