Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amefafanua sakata lake la kuchukuliwa na askari wa Takukuru kwa mahojiano muda mfupi baada ya kuchukua fedha benki, akisema alikuwa akielekea kulipa mawakala.
Nape,
anayewania ubunge wa Jimbo la Mtama, jana mchana a
liamriwa na maofisa wa Takukuru kufika ofisi zao baada ya kutoka kuchukua fedha benki ya NMB eneo la Misonobarini mkoa Lindi.
liamriwa na maofisa wa Takukuru kufika ofisi zao baada ya kutoka kuchukua fedha benki ya NMB eneo la Misonobarini mkoa Lindi.
“Ninadhani hawa jamaa walipotoshwa. Mimi nimekwenda zangu benki kuchukua fedha, lengo langu ni kuwalipa mawakala,” alisema Nape jana jioni .
“Wakaja
hawa jamaa, wakajitambulisha kuwa wanatoka Takukuru, wakaniuliza ‘mbona
ninachukua fedha nyingi kipindi hiki?’ Nikawaambia ‘nakwenda kulipa
mawakala, na fedha zenyewe ni hizi Sh3.6 milioni’.
“Basi,
tukatoka taratibu tukaenda ofisini kwao, ni karibu tu na benki.
Wakanihoji hata haikumalizika nusu saa, niliwaambia nataka kulipa
mawakala wangu, tena fedha zenyewe hazitoshi, wako zaidi ya 100.”
Nape aliongeza kusema kuwa walimkamata na akawaambia kuwa yeye ni mwadilifu.
“Halafu ninyi, mnaacha marushwa makubwa makubwa huko, watu wanahonga halafu mnamvizia Nape masikini kwa Sh3mil?,” alisema.
Nape
alielezea kufadhaishwa na tukio hilo akidai kuwa limetengenezwa kwa
ajili ya kumchafua hasa kwa kuwa leo kuna kura za maoni, lakini akasema
anaamini yeye ni msafi.
Kamanda
wa Takukuru wa Mkoa wa Lindi, Stephen Chami alikiri kumhoji Nape,
lakini akasema walijiridhisha kuwa fedha hizo ni kwa ajili ya kulipa
mawakala.
Post a Comment