Nikifungo ca mwaka mmoja kuto kwa
Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) limemfungia mwanamuziki Zuwena Mohamed ‘Shilole” kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na kukiuka sheria na maadili.
Barua ya BASATA imesomeka hivi “Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la
muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za
Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili”.
“BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA
lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila
kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa
maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini
umekaidi kutoa maelezo yako”.
"Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa
kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye
ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka
1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza
linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi
kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi
pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae”.
Post a Comment