Gabon
baada ya fujo kuzuka kuhusiana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.
Baraza la
Usalama la umoja huo limetoa wito kwa wagombea wakuu na wafuasi wake kujizuia
kufanya uchokozi na kutatua mzozo wa sasa kupitia njia za kisheria.
Maafisa
wa usalama kufikia sasa wamewakamata watu zaidi ya elfu moja baada ya
siku ya
pili ya maandamano ya wafuasi wa upinzani.
Upinzani
unadai Rais Ali Bongo aliiba kura wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi
Watu
watatu waliuawa mji mkuu Libreville.
Umoja wa
Mataifa umezihimiza kuwepo kwa utulivu nchini Gabon baada ya fujo kuzuka
kuhusiana na utata kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais.
Baraza la
Usalama la umoja huo limetoa wito kwa wagombea wakuu na wafuasi wake kujizuia
kufanya uchokozi na kutatua mzozo wa sasa kupitia njia za kisheria.
Maafisa
wa usalama kufikia sasa wamewakamata watu zaidi ya elfu moja baada ya siku ya
pili ya maandamano ya wafuasi wa upinzani.
Upinzani
unadai Rais Ali Bongo aliiba kura wakati wa uchaguzi huo uliofanyika Jumamosi.
Upande wa Bw Ping unasema takwimu
kutoka ngome za rais huyo zinaonyesha asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza.
Ameomba takwimu za wapiga kura kutoka kila kituo zitolewe wazi.
Bw Bongo aliingia madarakani mwaka
wa 2009, baada ya kifo cha babake aliyekuwa ameongoza taifa hilo tangu 1967.
Kabla ya kuingia katika siasa, Ping
aliwahi kuhudumu kama mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika
Matokeo ya uchaguzi yalitangazwa
Jumatano alasiri na kumpatia Bw Bongo ushindi kwa 49.8% ya kura, akifuatwa na
Bw Ping aliyepata 48.2 % ya kura, kura zilizowatenganisha zikiwa 5,594.
Bw Ping alisema uchaguzi huo ulijaa
udanganyifu na "hakuna ajuaye" hasa nani alishinda.
Waandamanaji waliingia barabarani
muda mfupi baada ya tangazo kutolewa. Walichoma moto majengo ya bunge na
kukabiliana na polisi wa kuzima fujo.
Upande wa Bw Ping unasema takwimu
kutoka ngome za rais huyo zinaonyesha asilimia 99 ya wapiga kura walijitokeza.
Ameomba takwimu za wapiga kura kutoka kila kituo zitolewe wazi.
Bw Bongo aliingia
madarakani mwaka wa 2009, baada ya kifo cha babake aliyekuwa ameongoza taifa
hilo tangu 1967.
Post a Comment