Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Septemba, 2016 amemteua Bw. Eliya Mtinangi Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.
Bw. Eliya Mtinangi Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana tarehe 09 Septemba, 2016 ambao ni Ado Steven Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na Bw. Tixon Tuliangine Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Wakati huo huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji 1 na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa 1 ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Godwin Emmanuel Kunambi - Manispaa ya Dodoma
2. Elias R. Ntiruhungwa - Mji wa Tarime
3. Mwantumu Dau - Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba
4. Frank Bahati - Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe
5. Hudson Stanley Kamoga - Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu
6. Mwailwa Smith Pangani - Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo
7. Godfrey Sanga - Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama
8. Yusuf Daudi Semuguruka - Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga
9. Bakari Kasinyo Mohamed - Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea
10. Juma Ally Mnwele - Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo
11. Butamo Nuru Ndalahwa - Halmashauri ya Wilaya ya Moshi
12. Waziri Mourice - Halmashauri ya Wilaya ya Karatu
13. Fatma Omar Latu - Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo
Wakurugenzi wa halmashauri wote 13 walioteuliwa wanatakiwa kuripoti Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mkoani Dodoma siku ya Jumanne tarehe 13 Septemba, 2016 kwa ajili ya kupata maelekezo zaidi.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Septemba, 2016
Post a Comment