maana kuna ajali imetokea matumbi ikihusisha daladala(DCM) la G/Mboto-Ubungo na Lori la Mizigo pamoja na Lori lililokuwa limebeba ng’ombe .Ajali imetokea pale kabla hujafika Tabata Matumbi Pale Darajani
Kwa mujibu wa mganga mkuu Hospitali ya Amana, Dr Stanley Binagi, watu wanne wamefariki dunia huku 25 wakijeruhiwa.
Inaelezwa kuwa, Chanzo cha ajali hiyo, ni Lori lililobeba Mchanga ambalo liliikuwa kwenye mwendo kasi, kwenda kuligonga Daladala hilo kwa nyuma, hali iliyopelekea Daladala hilo kukosa mwelekeo na kwenda kugongana na Lori lingine lililokuwa limepakia Ng'ombe waliokuwa wakipelekwa Pugu Mnadani.
Na hii ni tofauti alivyoenea asubuhi kwamba wamekufa watu watano na kupona watu watano tu
Post a Comment