Hii
ina maana kwamba ushahidi ulioandikishwa awali na upande wa mashtaka hauwezi
kutumiwa dhidi ya Bw Ruto na mwanahabari Joshua Sang.
Uamuzi
huo ni pigo kubwa kwa upande wa mashtaka unaoongozwa na Fatou Bensouda.
Upande
wa mashtaka ulikuwa na mashahidi sita waliokuwa wanahusisha Bw Ruto na ghasia
za baada ya uchaguzi za mwaka 2007-08, vilivyosababisha vifo vya watu 1,200,
walioondoa ushahidi wao.
Upande
wa mashtaka unasema walitishiwa au wakahongwa.
Majaji
wa rufaa wamebatilisha uamuzi wa awali wa majaji uliosema upande wa mashtaka
unaweza kutumia ushahidi uliowasilisha na mashahidi hao kabla yao kubadili nia.
„Ushahidi
ulioandikisha awali uliwasilishwa bila washtakiwa kupewa fursa ya kuwahoji na
kuwauliza maswali mashahidi hao,” amesema jaji wa mahakama ya rufaa Piotr
Hofmanski.
Source bbc
Post a Comment