Walioshuhudia w
anasema
wanamgambo hao walirusha makombora hayo usiku kucha na kuwa milipuko kadhaa
ilisikika karibu na uwanja mkuu wa ndege.
Hata hivyo hakuna
ripoti yoyote kuhusu majeruhi, lakini ripoti zinasema kuwa safari kadhaa za
ndege kuelekea Mogadishu zimefutiliwa mbali.
Uwanja wa ndege wa
Mogadishu unalindwa vikali na unakaribiana na kambi ya wanajeshi wa kulinda
amani wa muungano wa Afrika nchini Somalia.
Kikosi hicho cha
wanajeshi elfu ishirini na mbili wa muungano huo wanaunga mkono serikali ya
nchi hiyo katika harakati zake za kupambana na wanamgambo wa kiislamu.
Ofisi za umoja wa
mataifa pia ziko katika kambi hiyo sawa na ubalozi wa mataifa ya kigeni.
Kufikia sasa hakuna
kundi lolote ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo, lakini wapiganaji wa Al
shabaab walio na uhusiano na kundi la kigaidi la Al Qaeda, wamefanya
mashambulio kadhaa ya mabomu mjini humo.
Wakati huo huo
uchunguzi unaendelea kufuatia mlipuko wa bomu katika ndege moja ya abiria
iliyotokea tarehe mbili mwezi huu.
Mlipuko huo ulitokea
katika ndege inayomilikiwa na shirika la Daalo muda mfupi tu baada ya kuruka
kutoka uwanja huo wa ndege wa Mogadishu na kusababisha kifo cha mlipuaji huyo
wa kujitolea, hali iliyoilazimisha ndege hiyo kutua kwa dharura.
Watu kum na watano
wamekamatwa kuhusiana na shambulizi hilo la Ndege.
SOURCE BBC
Post a Comment