Polisi
pamoja na mashuhuda wa matukio hayo wameelezea mashambulio hayo ya kingono kuwa
yalitekelezwa karibu na eneo maarufu la Cathedral, ambalo lilikuwa limefurika
idadi kubwa ya makundi ya wanaume wenye asili na muonekano wa Kiarabu ama
Afrika Kaskazini.
Merkel
ametoa agizo la kufanyika uchunguzi wa kubainiukweli kuhusiana na madai hayo na
kisha kuwaadhibu wahusika, bila kujali asili yao ama historia za awali.
Meya
wa mji wa Cologne, Henriette Reker, ameonya juu ya hatua zitakazochukuliwa
akisa haki inafaa kutendeka bila ya kuwaelemea wakimbizi walioingia nchini
Ujerumani.
Ameitisha
mazungumzo ya dharura na maafisa wa polisi kuhusiana na mgogoro huo.
Polisi
wameahidi kuimarisha ulinzi.
SOURCE BBC
Post a Comment