0

Shambulizi linalokisiwa kuendeshwa na wanamgambo wa Taliban katika chuo kimoja kaskazini magharibi mwa Pakistan limesababisha vifo vya watu 20 na kuwajeruhi wengine 50.
Afisa mmoja wa kijeshi amesema kuwa ufyatuaji wa risasi umekwisha lakini wanajeshi wanaendesha uch
unguzi katika chuo hicho cha Bacha Khan kilicho eno la Charsadda.
Jeshi lilisema kuwa washambuliaji wanne waliuawa huku kundi moja la Taliban wakisema kwa washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walihusika kwenye shambulizi hilo.
Msemaji wa Taliban aliliambia shirika la habari la AFP kuwa shambulizi hilo ni la kulipiza kisasi oparesheni ya kijeshi dhidi ya ngome za Taliban.
Baadaye, kundi kuu la Taliban, Pakistan limekanusha madai kwamba wanachama wake walihusika na wakashutumu shambulio hilo.
Taliban waliwaua wanafunzi 130 kwenye shule moja katika mji ulio karibu wa Peshawar mwaka 2014.
Siku chache zilizopita baadhi ya shule katika mji wa Peshawar zilifungwa kufuatia ripoti kuwa wanamgambo walikuwa wakipanga mashambulizi.



source BBC

Post a Comment

 
Top