Zaidi ya viongozi wakuu mia moja wa kanisa la Kianglikana wametia saini barua ya kulitaka kanisa la Uingereza kutubu kwa kuwabagua wakristo wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, watu wanaoshiriki mapenzi na jinsia zote mbili na wale walio na jinsia mbili.
Barua hiyo inayoelekezwa kwa askofu mkuu wa Canterbury na York, inasema kuwa wakristo hao wamekuwa wakichukuliwa kama raia wa daraja la pili.
Mkutano wa viongozi wa makanisa yote ya kianglikana unaanza hapo kesho nchini Uingereza.
Mkutano huo unatarajiwa kutawaliwa na gumzo kuhusu jinsia huku wanachama wa kanisa hilo ambao wanapinga mapenzi ya jinsia moja sasa wanawataka Waanglikana kutubu kwa kuwatukuza viongozi wa kanisa hilo ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
SOURCE BBC
Post a Comment