Wakati Tanzania ikipongeza, kusifu na kushukuru uhusiano na
ushirikiano wake na Umoja wa Mataifa kupitia Mifuko na Mashirika
yake ya Maendeleo, imeutaka p
ia Umoja huo kutekeleza majukumu
yake kwa kuzingatia, kanuni, taratibu, sheria na misingi iliyojiwekea ili
iendelee kujijenga heshima.
Hayo yameelezwa jana jumatatu na Mwakilishi wa Kudumu
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, wakati
wa mkutano wa Bodi za Mashirika ya Umoja
wa Mataifa UNDP, UNFPA na UNOPS. Tanzania ni
mjumbe wa Bodi katika Mashirika hayo.
Katika siku ya kwanza ya mkutano , mkutano
uliofunguliwa na Mtendaji Mkuu wa UNDP, Bi Helen Clark,
Balozi Manongi amesisitiza kwamba,
ili Umoja wa Mataifa uendelee kujijenga heshima na
kuheshimika, unapashwa kutoruhusu watendaji wenye ajenda na
maslahi binafsi kufanya kazi katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa.
“ Umoja wa Mataifa wakati wote umekuwa sehemu na mdau
mkubwa katika uimarishaji na ujenzi wa utawala bora katika
nchi nyingi , Tanzania ikiwamo. Wajibu wa Umoja wa Mataifa utabaki
kuwa halali na wenye nguvu endapo wale ambao wamepewa dhamana
ya kutenda kwa niaba yake watatambua na kuheshimu imani na wajibu
uliotukuka ambao wamepwa kuutekeleza ” akasisitiza Balozi Manongi
Akaongeza kwamba, mashabiki hawapaswi kupewa nafasi, wala
kuvumiliwa na kuwa sehemu ya miongoni mwa watendaji wa chombo hicho wasipewe
nafasi, wala wasivumiliwe kuwa miongoni mwa watendaji wa chombo
hicho.
Akizungumzia kuhusu rasimu ya Taarifa ya Mpango
wa Utekelezaji kuhusu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Country
report) kwa kipindi cha 2016-2021) ambayo imewasilishwa mbele ya Wajumbe wa
Bodi wa UNDP, Balozi Manongi amesema, mapendekezo yaliyomo
kwenye rasimu na ambayo imeshirikisha wadau mbalimbali inajumuisha
mawazo na mapendekezo kutoka pande zote za Muungano na imetokana na
misingi ya ushirikiano kati ya UNDP na Serikali ya Tanzania.
Vile vile akasema rasimu hiyo imejumuisha vipaumbele
vinavyoainishwa katika Dira ya Taifa ya 2025 kwa upande wa Tanzania
Bara , Dira ya 2020 kwa upande wa Zanzibar, mkakati
wa kupunguza umaskini kwa pande zote za Muungano pamoja na
Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano.
“ Tunaishukuru UNDP- Ofisi ya Tanzania kwa ushirikiano wake katika
utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwano mikakati ya
kupunguza umaskini, ushirikiano huu umekuwa mzuri ingawa
unachangamoto zake” akasisitiza Balozi Manongi
Akaeleza kwamba, kutokana na umuhimu wa mwaka huu wa 2016 ambao
pamoja na mambo mengine ni kuanza kwa utekelezaji wa Agenda ya
Maendeleo Endelevu ( Agenda 2030) Tanzania itaendelea kushirikiana
kwa karibu na UNDP katika utekelezaji wa Agenda hiyo huku
mkazo ukiwa ni katika kupungua ama kuondoa umaskini uliokithiri
kwa makundi ya mbalimbali ya jamii hususani wanawake.
Akasema , Serikali imejipanga vema katika utekelezaji wa mipango
mbalimbali inayolenga katika kuboresha maisha ya wananchi wake.
Ikiwa ni pamoja na kutatua tatizo la uhamaji wa wananchi wake
kutoka vijijini na kwenda katika miji mikuu hususani vijana kwa lengo la
kutafuta ajira na hali bora ya maisha.
Akasema kuwa wajibu au madhumuni ya msingi UNDP
ni kupunguza umaskini, ni kwa sababu hiyo Tanzania ingependa kuiona UNDP
ikijielekeza zaidi katika jukumu lake hilo la msingi kama inavyoelekezwa
katika maazimio mbalimbali ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wa ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu zinazohusu maeneo
mbalimbali, Balozi Manongi amesisitiza kwamba UNDP inapashwa
kufanya kazi kwa karibu na kwa ushirikiano na Ofisi ya Taifa ya Takwimu
kwa kile alichosema ndicho chombo cha serikali chenye dhamana juu ya
masuala yote yahusuyo takwimu.
Na kwa sababu hiyo akasema Tanzania inaridhishwa na taarifa ya kwamba
UNDP itashirikiana na Ofisi hiyo ya Taifa ya Takwimu katika
Nyanja mbalimbali zikiwamo za uwezeshaji kwa lengo la kusaidia katika
uhuishaji wa takwimu.
Aidha Tanzania imesisitiza kuhusu umiliki katika
uendeshaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo pamoja na kiushauri
UNDP kuhakikisha kwamba fedha zinazotengwa kwaajili ya
miradi ya maendeleo zinakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa na si
vinginevyo
Post a Comment