0
Mgombea anayeunga mkono harakati za uhuru kwenye taifa la Taiwan,  Tsai Yingwen kutoka Chama cha Democratic Progressive Party (DPP) ameshinda uchaguzi wa urais nchini humo.
Chama tawala cha Kuomintang ambacho kinapendelea ushirikiano na upande wa bara wa taifa la China k
ilipoteza uchaguzi huo.
Baada ya nusu ya kura zote kuhesabiwa DPP kilionyesha kuongoza kwa kishindo kwa  zaidi ya asilimia 60 ya kura zote zilizopigwa.
Tsai atakuwa Rais wa kwanza mwanamke kwenye dunia ya wazungumzaji wa lugha ya Kichina.
Pia kiongozi huyo anatarajiwa kutoa hotuba yake baada kutangaza rasmi kuwa kiongozi wa taifa hilo.
Kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huo nchini humo wachambuzi mbalimbali wa  kisiasa,  walisema kuna uwezekano mkubwa wa mgombea huyo  kushinda,  kinyume na matarajio ya raia wa China. Tsai halikuwa mwiba kwa Wachina kutokana na sera zake zinazoshinikiza uhuru wa kisiwa hicho dhidi ya mwingiliano wowote wa kisiasa.
Inaelezwa kwamba wapigakura wengi nchini humo hawakufurahishwa na ushirikiano wa karibu wa kisiasa na China, kwa madai haujawanufaisha kwa lolote’.
“Wapigakura wengi walihisi   mikataba ya kiuchumi ambayo imetiwa sahihi kati ya Taiwan na China  haijawanufaisha hata kidogo,” alisema mchambuzi  mmoja.
Ni mwanamke wa kwanza kuongoza Taifa hilo na anakabiliwa na changamoto nyingi kutoka kwa wapinzani wake.
SOURCE  Mwananchi


Post a Comment

 
Top