NaibuWaziriwaAfya, MaendeleoyaJamii, Jinsia, WazeenaWatotoMhe. Dkt HamisKigwangalla amezindua rasmi duka la Dawa la MSD jijiniArusha, ambalo liko ndani Hospitaliya Mount Meru na kuiagiza MSD mbali na kuweka alama ya GoT kwenye vidonge vyake iangalie pia utaratibu wa kuweka rangi maalumu kwenye vidonge na vifungashio, ilikurahisha udhibiti wa upotevu na ufuatiliaji wa dawa hizo.
Naibu Waziri huyo pia amewahimiza watendaji wa MSD kuwa waadilifu, kuwajali na kuwasilikiza wateja na kutumia lugha nzuri wakati wa kuwahudumia wateja, huku akitoaangalizo kwa wale wanao kiuka taratibuza ajira kuwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Kwa upande Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhaminiya MSD Prof. IdrisMtulia ameeleza kuwa MSD inaweza kufanya vizuri zaidi endapo changamoto za sheria ya manunuzi, mgawo mdogo wafedha kwa vituo vya Afya, hospitali na zahanati, na mgawo wafedha kuja kwa mafungu zitafanyiwa kazi.
Naye Mkurugenzi Mkuuwa MSD Bwana Laurean Bwanakunu ameeleza kuwa MSD itakuwa na maduka manne tu mkoani Dares Salaam, Mwanza, A Arusha na Mbeya ambapo kwa mikoa mingine MSD wanaafanyama wasiliano na hospitali za mikoa ziwe na maduka ya hospitali wanayoendesha wenyewe na kisha MSD iwauzia dawa na kuwawezesha utaalamu wakuendesha maduka hayo
Post a Comment