atakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi? Amehoji Simbeyi.
Amesema hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.
“Wanaiogopa mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa lazima iyakuwa na mapungufu yake tunacho hitaji ni mikutano uoneshwe live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.
Mbali na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.
Post a Comment