0
Kuwait sasa rasmi inaingia kwenye ugomvi Iran baada ya kutangaza kwamb
a kumuondoa balozi wake kutoka Iran huku mvutano kuhusu kuuawa kwa mhubiri wa Saudi Arabia nchini Saudi Arabia ukizidi.
Ubalozi wa Saudi Arabia nchini Tehran ulivamiwa na kuchomwa moto na waandamanaji waliokuwa wakilalamikia kuuawa kwa mhubiri wa madhehebu ya Shia Sheikh Nimr al-Nimr na watu wengine 46 nchini Saudia Jumamosi.
Saudi Arabia ilivunja uhusiano na Iran baada ya tukio hilo, na washirika wake wa karibu Bahrain na Sudan wakafuata.
 Marekani UN na Uturuki ni miongoni mwa nchi zilizohimiza kuwepo kwa utulivu Mashariki ya Kati.

Saudi Arabia na Iran ndizo nchi kuu za Kisuni na Kishia mtawalia eneo la Mashariki ya Kati na zimekuwa wapinzani wakuu.
Nchi hizo huunga mkono pande pinzani katika mizozo Syria na Yemen.

Post a Comment

 
Top