Virusi vya HIV
vimeanza kuwa na kinga dhidi ya dawa ya Tenovir katika asilimia 60 ya visa
vyote miongoni mwa mataifa kadhaa ya Afrika kulingana na utafiti huo
uliofanyika kati ya mwaka 1998 na 2015.
Utafiti huo
,ulioongozwa na chuo kikuu cha London,uliwashirikisha takriban watu 2000 walio
na virusi hivyo duniani.
Kiongozi wa
utafiti huo Daktari Ravi Gupta amesema kuwa matokeo yake yalizua wasiwasi
mkubwa.
Kazi hiyo
iliochukua miaka minne kukamilisha.Ilianza mwaka 2012 na iliwalinganisha
wagonjwa wa ugonjwa huo barani Afrika na wale wanaoishi barani Ulaya.
Huku wagonjwa
hao wakigawanywa katika makundi mawili,utafiti huo ulibaini kwamba barani
Afrika asilimia 60 ya wagonjwa walikuwa hawatibiki na dawa ya Tenovir huku
barani Ulaya idadi hiyo ikipungua na kuwa asilimia 20.
Matokeo hayo ambayo yamechapishwa katika
jarida la Lancet kuhusu magonjwa ya maambukizi,ulisema kuwa usimamizi m'baya wa
dawa hizo kama vile kutozitumia zinavyohitajika na katika viwango vilivyo sawa
huenda ndio sababu ya tatizo hilo.
''Iwapo viwango
sawa vya dawa hiyo havitatumika ,virusi vinaweza kukabili dawa hiyo na kuwa na
kinga'',Daktari Gupta aliiambia BBC.
''Tenovir ni
dawa muhimu katika vita dhidi ya virusi vya ukimwi,kwa hivyo inatia wasiwasi
sana kuona viwango vya virusi vilivyo na kinga dhidi ya dawa hiyo'',aliongezea.
Utafiti huo pia
umesema kuwa virusi vilivyo na kinga dhidi ya Tenovir vinaweza kusambazwa
kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine.
Post a Comment