0
Ukifanya ubaya utalipwa ubaya na muda mwingine hukumu duniani hapa hapa hii imejidhiirisha baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya R
wanda (ICTR) imeamua waziri mmoja wa zamani wa Rwanda atumikie kifungo cha miaka 47 jela kwa mchango wake mauaji ya kimbari ya 1994.
Pauline Nyiramasuhuko ni mmoja wa washtakiwa sita waliokuwa wamekata rufaa kwenye mahakama hiyo maalum ambayo imemaliza kazi yake.
Alikuwa amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani awali, lakini mahakama ikaamua kupunguza adhabu dhidi yake, sawa na adhabu dhidi ya Arsène Shaim Ntahobali na Elie Ndayambaje.
Kesi hizo zilikuwa za mwisho kusikizwa na mahakama hiyo kabla ya kufungwa rasmi baada ya kusikiza kesi dhidi ya washukiwa wa mauaji hayo kutoka mjini Arusha, Tanzania kwa miaka 21.
SOURCE BBC


Post a Comment

 
Top