KWA mara ya
kwanza Lugha ya Kiswahili imeingia katika rekodi ya dunia kwa watanzania wanne
kuchomoza katika tuzo ya waandishi ya Fasihi Afrika.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mshiriki wa Taaluma ya
Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa, Adrian
Mtembei amesema lugha
ya Kiswahili ya kujivunia kutokana na watanzania wenye lugha yao kuwa washindi.
Washindi wa
tuzo hizo ni Enock Maregesi ambaye aliandika Kolonia Santita,Chiristophee
Bubebah, Anna Manyaza aliandika Penzi la Damu, Mohamed Ghassani aliandika N’na
Kwetu.
Walioshiriki
katika tuzo hiyo walikuwa 65 na kuweza kuibuka watu wanne ambao ni washindi
wakitokea nchini na sherehe hizo zilifanyika Nchini Kenya.
Amesema kwa
lugha ya kifaransa na Kiingereza zimekuwa zikijitokeza kila mwaka kwa watu
kuandika riwaya na mashairi lakini Kiswahili imekuwa ikisahaulika hivyo na
kufanya Chuo Cornell Nchini Marekani iliamua kufanya hivyo kuwa watu kuandika
Riwaya na Mashairi.
Katika tuzo
hizo Kampuni ya watengenezaji wa Mabati ya Alaf ilizamini tuzo hizo na kutaka
watu wajitokeze katika kuinua lugha ya Kiswahili duniani.
Afisa Masoko
wa Alaf, Theresia Mmasy amesema kazi wataendelea kushirikiana na watanzania
katika kukuza Kiswahili katika kudhamini tuzo hizo.
Post a Comment