Sasa inajiziilisha watu kufanya mambo bila kumuoga tena raisi John Pombe Magufuri Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Juma Assad aliondoka nchini Jumamosi (Desemba 12, 2015) kwenda jijini Nairobi, Kenya na kurejea nchini Jumanne wiki hii.
Taarifa hizo, zimesema CAG alikwenda kutoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kazi ambayo haina uhusiano na ofisi yake, lakini alilipiwa gharama zote na ofisi yake.
“Bosi wetu aliondoka kwenda Nairobi Jumamosi iliyopita na kurejea Jumanne, alikwenda kutoa mhadhara katika Chuo Kikuu cha Nairobi bila kibali cha Ikulu, alipaswa kupata kibali kwa sababu ofisi yake ndio ililipa gharama zote.
“Jumla ya gharama zinafika Sh milioni 15, ambazo ni pamoja na posho, tiketi ya ndege, hoteli na gharama nyinginezo,” kilisema chanzo cha gazeti hilo.
Alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu safari hiyo, Profesa Assad hakuthibitisha wala kukanusha taarifa hizo, zaidi ya kutishia kwenda mahakamani.
“Wewe si umesema umepata taarifa kutoka vyanzo vyako na umenipigia ‘for validation’, sasa mimi nakwambia hizo taarifa si za kweli na mkiandika tutachukua hatua,” alijibu CAG.
Baada ya muda, Profesa Assad alipiga simu kwa mhariri akimtaka afike ofisini kwake akachukue nyaraka za kuthibitisha kuruhusiwa na kusafiri nje ya nchi na ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Kutokana na mhariri huyo kuwa nje ya Dar es Salaam, alimtuma mwandishi mwingine kwenda katika ofisi ya CAG ili kuchukua nyaraka hizo. Mwandishi alipofika, CAG alikataa kumpa wala kumwonesha nyaraka hizo.
Juhudi za kumpata Balozi Sefue kuzungumzia suala hilo hazikuzaa matunda. Baada ya kupigiwa muda mrefu aliandika ujumbe mfupi wa simu ukisema. “Nimebanwa na majukumu siwezi kupokea simu yako,”ulisomeka ujumbe huo.
Tukio hilo la CAG limekuja siku mbili baada ya Rais Dk. John Magufuli kuagiza kusimamishwa kazi kwa watumishi wanne wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa kosa la kusafiri nje ya nchi bila kibali cha Ikulu.
Watumishi wa taasisi hiyo waliosimamishwa kazi ni Ekwabi Mujungu (Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu), Doreen Kapwani, Rukia Nikitas na Mary Mosha.
Profesa Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Novemba 5, 2014.
Kabla ya uteuzi wake, alikuwa Profesa Mshiriki, Idara ya Uhasibu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na alichukua nafasi ya Ludovick Utouh ambaye alistaafu kwa mujibu wa sheria.
Related Posts
VIONGOZI WA DINI WA WASHAMBULIA CHADEMA
Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi[...]
Sep 24, 2016KWA USHUJAA HUU CHADEMA WANATAKIWA KUIGWA
September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke kimemfukuza uanachama[...]
Sep 24, 2016LIPUMBA APEWA WENYEKITI CUF
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Prof. Ibrahim Lipumba bado[...]
Sep 24, 2016CUF WAJIBU BAADA YA LIPUMBA KUTANGAZWA KUWA MWENYEKITI
Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza[...]
Sep 24, 2016NCHI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE IMEZUKA KANANGA
Ghasia za siku mbili katika mji wa Jamhuri ya kidemorasi ya Congo zimesababisha vifo vya watu 10.[...]
Sep 24, 2016BODI YA HABARI WA MWACHIA UONGOZI RAISI MAGUFURI
Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavy[...]
Sep 24, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.