Mahakama
Kuu nchini Rwanda imemhukumu kifungo cha maisha jela mhubiri aliyehusika katika
mauaji ya kimbari ya 1994.
Jean Uwinkindi
alipatikana na hatia ya kupanga na kushiriki katika mashambulio dhidi ya
Watut
si, mahakama ilisema.
Mchungaji huyo wa
umri wa miaka 64, kutoka jamii ya Wahutu, ndiye mshukiwa wa kwanza wa mauaji ya
kimbari kutumwa Rwanda akajibu mashtaka na iliyokuwa mahakama maalum ya UN
iliyoendesha shughuli zake kutoka Arusha, Tanzania.
Uwinkindi, aliyekuwa
kiongozi wa kanisa la kipentekoste viungani mwa mji mkuu Kigali, alikuwa
amepinga kurejeshwa kwake Rwanda.
Alisema hangepata
hati Rwanda, ambayo sasa inaongozwa na Watutsi.
Mawakili wake
wamesema atakata rufaa uamuzi huo wa mahakama huu.
“Mahakama imebaini
kwamba kulitokea mauaji ya Watutsi katika milima ya Rwankeri and Kanzenze na
mashambulio hayo yaliongozwa na Uwinkindi," alisema Jaji Kanyegeri
Timothee, kama alivyonukuliwa na shirika la habari la Reuters.
Upande wa mashtaka
uliambia mahakama kwamba uchunguzi uliofanywa baada ya mauaji hayo uligundua
miili 2,000 karibu na kanisa hilo la Kanzenze.
Uwinkindi
alifunguliwa mashtaka 2011 baada ya kukamatwa 2010 katika nchi jirani ya
Uganda.
Mshukiwa mwingine
mkuu, Ladislas Ntaganzwa, alikamatwa wiki mbili zilizopita nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
SOURCE BBC
Post a Comment