Shirika rasmi la
habari la Saudi Arabia limesema kazi ya muungano huo itaratibiwa katika kituo
cha pamoja mjini Riyadh.
Wajumbe
wa muungano huo ni mataifa ya kiarabu, Afrika na Asia Kusini .
Akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari, waziri wa ulinzi wa Saudia , Mwanamfalme
Mohammed bin Salman, amesema kua muungano huo utaratibu juhudi za mapigano
dhidi ya makundi yenye itikadi kali katika mataifa ya Syria, Iraq, Libya, Misri
na Afghanstan .
Hata hivyo kuna
taarifa chache kuhusu namna kikosi hiki kitakavyotekeleza majukumu yake.
Mataifa ya ghuba
yanakabiliwa na shinikizo kufanya juhudi zaidi katika vita dhidi ya kundi la
Islamic State nchini Iraq na Syria
Orodha ya mataifa katika
muungano huo
§
Saudi Arabia,
§
Bahrain,
§
Bangladesh,
§
Benin, Chad,
§
Comoros,
§
Djibouti,
§
Misri,
§
Gabon,
§
Guinea,
§
Ivory Coast,
§
Jordan,
§
Kuwait,
§
Lebanon,
§
Libya,
§
Malaysia,
§
Maldives,
§
Mali,
§
Morocco,
§
Mauritania,
§
Niger,
§
Nigeria,
§
Pakistan,
§
Palestina,
§
Qatar,
§
Senegal,
§
Sierra Leone,
§
Somalia,
§
Sudan,
§
Togo,
§
Tunisia,
§
Uturuki,
§
Milki za Kiarabu
§
Yemen.
Post a Comment