KATIBU wa NEC (CCM) Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye leo ametembelea
ofisi za kampuni ya Raia Mwema inayotengeneza magazeti ya Rai
a Mwema na Raia
Tanzania, kwa lengo la kushukuru na kueleza mikakati ya chama chake
.
Itakumbukwa miezi kadhaa
iliyopita kabla ya uchaguzi mkuu Nape, alitembelea vyumba vya habari akianzia
na Raia Mwema kueleza pamoja na mambo mengine namna walivyojipanga na uchaguzi
ikiwemo kupata mgombea urais.
Akizungumza jana katika ofisi hizo alipokutana na wahariri pamoja
na viongozi mbalimbali wa kampuni hiyo alisema, wanafurahishwa na kasi ya Rais
John Magufuli, kwa sababu kinachotendeka sasa walikipanga hata kabla ya
uchaguzi.
“Tulitaka mtu wa aina hii, haya mabadiliko tuliyarataji hivyo
hatushituki kuyaona, tunachotaka kuwaambia wananchi tu ni kuwa baada ya
kumaliza serikalini mabadiliko yatahamia kwenye chama,” alisema Nape.
TAZAMA VIDEO
TAZAMA VIDEO
Mhariri Mkuu wa Magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania Ndugu Godfrey Dilunga akiwatambulisha baadhi ya viongozi wa kampuni ya Magazeti ya Raia Mwema.
Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati wa kikao na wahariri wa magazeti ya Raia Mwema na Raia Tanzania.
Post a Comment