Dk Hamisi
Kigwangalla ameagiza kubadilishwa kwa mifumo ya utawala, malipo na uendeshaji
katika katika hospitali nchini ili kuleta ufanisi na tija.
Akizungumza
katika ziara yake ya kujifunza kuona katika hali ya kawaida huwa zinatolewaje
katika
hospitali za wilaya na mikoa alisema kukosekana kwa mifumo bora ya
malipo na motisha kumedumaza utumishi.
Ziara yake
hiyo ambayo aliifanya katika hospitali ya mkoa wa Lindi ya Sokoine na Ile ya
Mtwara ya Ligula ililenga kuona masuala mbalimbali yanayohusiana na utoaji
huduma ili kuwa na nafasi ya kutengeneza hali bora zaidi kimkakati.
Alisema
tatizo la upungufu wa dawa na hata raslimali watu linasababishwa na kukosekana
kwa mfumo waukusanyaji mapato ulio sahihi na wenye salama ambao utawezesha pia
kutoa motisha mbalimbali kwa watumishi ili kuwavutia kufanyakazi katika mikoa
ya pembezoni.
Naibu Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee, Dkt. Hamisi Kigwangalla
akipewa maelezo na Kaimu Muuguzi Mkuu wa Hospitali ya Sokoine ya Mkoa wa Lindi,
Damasiana Msalla alipotembelea wodi ya wazazi na kuridhishwa na huduma za
hospitalini hiyo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya mwishoni mwa juma
mkoani Lindi.
Aidha alisema
malipo yanayofanyika katika hospitali hizo yanatakiwa kuwa ya kielektroniki kwa
kuwa imethibitishwa kila kunapokuwapo na mfumo wa malipo kielektroniki
unaboresha mapato na hatimaye kuboresha ufanisi katika uendeshaji wa hospitali
pamoja na kuwapo kwa huduma bora za dawa.
Pia ameagiza
kuharakishwa kwa mfumo wa malipo kielektroniki kwa wateja wa Bima ili mchango
wao usaidie kwa haraka utoaji wa huduma ndani ya hospitali.
Hata hivyo
Naibu Waziri huyo alisema aliridhishwa na utendaji katika hospitali ya Sokoine
na Ligula na kusema ufanisi wao unatokana na kuwapo kwa mipango inayowezesha
kazi kufanywa.
Post a Comment