Mvutano wa hoja Nape
Nauye na Freeman
Mbowe kuhusu utendaji wa kazi magufuri kwa upande wake mbowe amesema “anafurahi kuona Rais John Magufuli
akitek
eleza sehemu kubwa ya sera za chama chake na kwamba kazi ya upinzani si
kupinga kila kitu, bali kuangalia masilahi mapana ya Taifa.
“biashara imeisha” kwa Rais John Magufuli
baada ya kutoka kwenye kikao cha Kamati Kuu ya CCM kwa kuwa chama hicho
kilimdhibiti katika uteuzi wa Baraza la Mawaziri kiasi cha kumfanya arudishe
sura zilezile.
Rais ameanza kazi kwa
kishindo baada ya kufumua uozo kwenye taasisi mbalimbali za Serikali kama
Mamlaka ya Bandari (TPA), Mamlaka ya Mapato (TRA), Hospitali ya Taifa Muhimbili
(MNH), huku akidhibiti matumizi ya Serikali kwa kubana safari za nje za
watumishi wa umma, kuondoa posho za vikao na pia kuanza utekelezaji wa ahadi ya
elimu bure.
Mbowe anaona mambo hayo
ndiyo ambayo wapinzani wamekuwa wakipigia kelele wakati wote.
Alitaja mambo hayo kuwa
ni hoja ya kubana matumizi ya Serikali, kupunguza safari za nje za viongozi na
kupunguza idadi ya watumishi wasio wa lazima.
Mambo mengine alisema ni
kupunguza sherehe za kitaifa na kuwa na Serikali ndogo. Alisema kwa kiasi
kikubwa Rais anatekeleza sera za upinzani ambazo zilikuwa zinapingwa na wabunge
wa CCM”.
Mbunge huyo wa Hai
aliongeza kuwa Kambi Rasmi ya Upinzani itaendelea kutimiza wajibu wake wa
kusimamia mambo yenye masilahi kwa wananchi na haitaona haya kuikosoa Serikali
pale inapotoka kwenye mstari.
Dk Magufuli ameanza urais
kwa kufuta safari za nje hadi kwa kibali cha Ikulu, kumuondoa kaimu mkurugenzi
mtendaji wa MNH na kuvunja bodi ya hospitali hiyo, kumuondoa kamishna mkuu wa
TRA, mkurugenzi mkuu wa Takukuru, mkurugenzi mkuu wa TPA na katibu mkuu wa
Wizara ya Uchukuzi kutokana na udhaifu alioukuta kwenye taasisi zao. Pia,
ameanza kutekeleza ahadi ya elimu bure kwa kuagiza walimu wakuu kutolipisha
wanafunzi ada kuanzia Januari na kufuta michango ya aina yoyote shuleni.
Pia, ametangaza Baraza la
Mawaziri lenye watu 34, kufuta sherehe za maadhimisho ya Uhuru, Siku ya Ukimwi
na kupongeza wabunge, akielekeza fedha zilizopangwa kwa shughuli hizo
kuelekezwa katika kutatua matatizo ya wananchi.
Mbowe pia hakusita
kukosoa Baraza la Mawaziri lililotangazwa na Dk Magufuli.
“Hakuna kipya,” alimalizia
kusema Mbowe.
“Sura ni zilezile
zilizokuwapo kwenye Serikali iliyopita na baadhi ya mawaziri wanakabiliwa na
kashfa.”
Mwenyekiti huyo alitoa
mfano mfano wa uteuzi wa Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe
kwamba haukuwa sahihi kwa sababu ndiye aliyeteua bodi ya Bandari ambayo
imevunjwa na Rais kutokana na usimamizi mbovu.
Aliongeza kuwa kurudi kwa
Profesa Sospeter Muhongo pia si sahihi kwa sababu aliondolewa kwa uamuzi wa
Bunge kutokana na kashfa ya uchotwaji fedha kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow.
Alisema Baraza la
Mawaziri halina jipya kwa sababu Rais Magufuli alidhibitiwa na Kamati Kuu ya
CCM katika kuliunda.
“Rais alifungwa mikono na
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi na tangu ametoka Kamati Kuu biashara
imeisha,” alisema Mbowe.
Lakini Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye alimjibu Mbowe kuwa walitegemea kauli
kama huyo kutoka kwa mwenyekiti huyo wa Chadema.
“Mwenyekiti wa Chadema
angesifia uteuzi wa Baraza la Mawaziri, ningeshangaa sana,” alisema Nape,
ambaye ni pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.
“Alichokisema ndicho
wengi tulichokitarajia. Maoni ya Mbowe ni ushahidi wa jinsi asivyojua hata
Katiba ya nchi inayoeleza mamlaka ya Rais juu ya uteuzi wa Baraza la Mawaziri
kuwa haingiliwi na yeyote.
“Namshauri arudi shule
kwa kuwa itamsaidia kuelewa kidogo.”
Post a Comment