Arusha amechinjwa kama kuku kwa Mkuu wa Idara ya Upelelezi ya Ulinzi wa
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Stephen Kisamo. Na mpaka sasa polisi
mkoani arusha Imewaweka chini ya ulinzi watu wawili wanao usishwa na mauaji hayo.
Habari kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Arusha zilieleza tayari
imewatia ndani watu wawili ambao ni marafiki wakubwa wa Kisamo na wanajua siri
nzito kutokana na kunaswa kwa mawasiliano ya simu ya kiganjani kati ya marehemu
na watu fulani muda mfupi kabla ya mauti kumfika ambao polisi inawachunguza kwa
karibu.
“Wasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas
sisi tumeshakamata watu wawili wa karibu na marehemu na sms na mawasiliano
yanatia shaka, lakini ukweli utajulikana muda si mrefu,” kilieleza chanzo chetu
cha habari ndani ya Jeshi la Polisi.
Kamanda Sabas alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Desemba 18,
mwaka huu asubuhi katika eneo la Kikwakwaru jijini Arusha muda mfupi baada ya
Kisamo kutoka nyumbani kwake akiwa na gari aina ya Mazda.
Sabas alisema siku hiyo hiyo jioni alifika kituoni hapo mke wa
marehemu na kueleza juu ya kutoweka kwa mumewe ambapo mara moja polisi walianza
kufuatilia jambo hilo bila mafanikio.
Kamanda Sabas alisema usiku, Polisi ilipokea taarifa kutoka kwa
raia wema wa eneo hilo la Kikwakwaru kuhusu kuonekana kwa gari hilo likiwa
limeegeshwa maeneo hayo kwa muda mrefu bila kuonekana mtu yeyote ambapo
walifika na kulikuta gari hilo, lililovutwa hadi katika Kituo Kikuu cha Polisi
usiku huo na baadaye lilitambuliwa na mke wa Kisamo.
Baadaye walirejea eneo la tukio kwa lengo la kutafuta mwili wa
marehemu huyo, lakini hawakufanikiwa kuupata mwili wala kumuona kachero huyo
ambapo walilazimika kuomba ruhusa ya kupekua gari hilo.
Alisema baada ya kuomba ruhusa hiyo, mke wa marehemu
alipowasilisha ufunguo wa akiba wa gari na Polisi walipofungua na kuanza
upekuzi walikuta mwili wa marehemu ukiwa umekunjwa kwenye buti, huku shingo
yake ikiwa imechinjwa eneo la nyuma ya shingo yake.
Aidha, Kamanda Sabas alisema kwa mujibu wa maelezo ya mkewe,
mumewe alikuwa mgonjwa na alikuwa akijiandaa kwa safari ya India kwa matibabu,
hivyo kabla ya tukio walidhani alitekeleza gari baada ya kuzidiwa na ugonjwa.
Watanzania wote tuungane tusiwe kama
wanyama kwani sisi sote ni ndugu wa baba mmoja haya mauji ya kinyama ya fike
mwisho
Post a Comment