Vikao ambavyo Maalim Se
if amekuwa akishiriki
pamoja na Dk. Shein, ndani ya Ikulu ya Zanzibar, vimehusisha pia marais
wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma na Amani Abeid Karume, ambaye
alishirikiana naye kujenga siasa za maridhiano kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka
2010.
Hakuna taarifa iliyotolewa na upande wowote
baada ya kikao cha Maalim Seif na Rais Magufuli, lakini mazingira yanaonesha
kuwa ni hatua za dhati za kiongozi huyo mpya za kusimamia utatuzi wa mgogoro wa
Zanzibar.
Rais Magufuli aliahidi wakati wa kuzindua
Bunge la 11 mjini Dodoma kuwa kuna tatizo linapaswa kushughulikiwa Zanzibar na
mbali na makamu wake wa rais, Samia, atashirikiana na Dk. Shein.
Mkutano wake na Maalim Seif unafanyika
katika wakati ambao wananchi wamekuwa wakisubiri kwa shauku kubwa kujua hatima
ya mgogoro uliotokana na hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC), Jecha Salim Jecha kuufuta uchaguzi wa Zanzibar uliofanyika Oktobva 25.
Taarifa yake hiyo imepingwa kwa nyanja
mbalimbali, ikianzia na wanasheria wa ndani ya Tanzania, serikali za kimataifa
na wananchi, wakisema hakuna mamlaka yoyote ya kisheria yanayompa haki ya
kufanya hivyo.
Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS)
kimesema Jecha hana mamlaka hayo kwa sheria yoyote wala katiba ya Zanzibar, na
anapaswa kufuta tamko lake ili Tume ikamilishe kazi ya kuhakiki kura
zilizobakia na kutangaza matokeo yake pamoja na mshindi wa nafasi ya urais.
Alipotoa tangazo la kufuta uchaguzi Oktoba
28, Jecha alikuwa ameshatangaza matokeo ya urais ya majimbo 33, ambayo wawakilishi
wake walishapatiwa vyeti vya ushindi pamoja na majimbo mengine yote yaliyobaki.
Zanzibar ina majimbo 54 ya uchaguzi.
Maalim Seif na chama chake Chama cha
Wananchi (CUF) wanasema Jecha alishinikizwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM)
kuufuta uchaguzi baada ya kuthibitisha kuwa kilishapoteza madaraka kwa
kushindwa uchaguzi.
CCM imekuwa ikishikilia kuwa Tume itangaze
tarehe ya kufanyika uchaguzi mpya, shinikizo ambalo watendaji wa Tume wanasema
hawawezi kulifanyia kazi kwa kuwa hawajapatiwa fedha za maandalizi ya uchaguzi
huo.
Post a Comment