Wabunge wadodoma watokea kutokuona umuhimu wa wa wakuu
wilaya na mkoa na kusema ya fuatayo na hi ni baada ya Paul Makonda kutupa
lumande watumishi wa umma wamesema “Inasikitisha kuona wakuu wa Wilaya na Mikoa
wanavyokuru
puka kwa sasa kuwawajibisha watendaji ambao wapo chini yao kwa
kuwanasa vibao ama kuwasweka rumande.
“Hapo utajiuliza muda wao walikuwa wapi
hata hivyo ukiangalia vizuri utagundua wazi kuwa wakuu wa
Mikoa na Wilaya hawana kazi yoyote ya
kufanya na badala yake watendaji wakuu ni Makatibu tawala wa Mikoa au
wakurugenzi wa Halmashauri husika” amesema Mbunge huyo.
Wabunge wakipendekeza hayo baadhi ya
watumishi katika halmasauri ya Dodoma,nao kwa masharti ya kutokutaka kutajwa
majina wamesema kwamba kutokana na kasi ya utendaji wa Rais Magufuli sasa
wanasiasa wanalazimisha kuingilia masuala ambayo ni ya kitaalam.
“Tunashangaa zaidi kuona wanasiasa kama
vile wakuu wa wilaya na wakuu wa Mikoa wakiwakaripia watumishi ambao ni
wanataaluma.
“Na pale wanasiasa wanaposhauriwa juu ya
utendaji wao wanakuwa wakali wakali zaidi kwa sasa kilichobaki ni watumishi
kukaa kimya ili wawasikilize wanasiasa lakini matokeo yake kazi zitalala”
alisema Mtumishi huyo.
Yapo mambo mengine kwa sasa ambayo uwezi
kuyafanya kutokana na kuhitajika kwa vitendea kazi,wakati mwingine unatakiwa
kutoa tiba wakati huo hakina vifaa.
Watumishi hao wanalazimika kutoa yao ya
moyoni kutokana na taarifa mbalimbali zinaziripotiwa kuwa wapo baadhi ya wakuu
wa Wilaya na wakuu wa Mikoa ambao wanawazaba watumishi vibao na kuwashweka
ndani watumishi.
Pia wanasheria
mkoani Dodoma wamesema ya moyoni wamewataka
baadhi viongozi wa serikali kuacha kutumia madaraka yao vibaya kwa kuwadhibu
baadhi ya watumishi wanaochelewa kazini kwani kufanya hivyo ni kosa.
Siku za hivi karibuni vyombo vya habari
kumezagaa taarifa za baadhi ya viongozi ndani ya serikali wamedaiwa kutumia
nyadhifa zao vibaya kwa kuwapiga au kuwasweka lumande watumishi wa ngazi ya
chini pindi wanapobainika kuchelewa kufika kazini.
Wanasheria hao kwa kuweka weka sawa
suala la wakuu wa mikoa na wilaya au kiongozi yotote kumpiga mtumishi walisema
kwa kufanya hivyo ni kosa la jinai.
Hii ikiwa ni baada ya Paul makonda
kusweka ndani maafisa ardhi waliochelewa kazini
Post a Comment