0
1
kimia Cha Magufuri kuchelewa kutangaza baraza ni hofu aliyonayo kuangushwa na mawaziri anataka watu watakao endana na kasi yake katika utendaji anahofu ya kuangushwa na Mawaziri laini mpkaka  ni siku ya 28 wakati mkapa alitumia siku 5 tu

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaeleza kwamba kwa sasa Rais Magufuli, anasuasua kutangaza baraza lake kutokana na kile kinachodaiwa ni kuandaa mikataba ambayo mawaziri baada ya kuteuliwa watalazimika kuisoma kwa muda wa siku mbili kabla ya kukubali uteuzi huo.


“Kwa sasa huyu jamaa anaandaa mikataba kwa ajili ya kuwapatia Mawaziri na Manaibu wake na wanatakiwa kuisoma ndani ya siku mbili na yeyote atakayekubaliana na mkataba huyo atalazimika kuisaini.






“Kitendo kinachofanywa na Rais Magufuli ni sawa na kumvua nguo Kikwete (Rais Mstaafu Jakaya Kikwete) kwani kwa madudu ambayo yanaonekana inaonesha wazi kuwa nchi haikuwa na kiongozi na kama ilikuwa na kiongozi basi kiongozi huyo alikuwa na mkono wake.

“Sikiliza kijana haiwezekani nchi ikawa na wafanyabiashara wakubwa na matajiri wakubwa wanaokwepa kodi huku kiongozi wa nchi kwa kujua ama kutokujua anakaa nao meza moja kwa kuwapongeza kwa misaada kiduchu wanayotoa katika jamii huku wafanya biashara hao wakiongeza wigo waliyonacho na wasiyonacho jambo ambalo ni hatari,” kilisema.

Wakati huo huo kuna tetesi kuwa kutokana na kasi ya Rais Magufuli kwa sasa ndani ya CCM kuna mvutano mkubwa ambapo wanataka kubadilisha katiba ya chama hicho.

Mgongano uliopo kwa sasa ndani ya Chama ni kutaka kubadilisha katiba ya chama hicho ili rais asiwe mwenyekiti wa chama.

“Hofu hiyo inatokana na kasi ya Rais Magufuli na inasemekana akiwa mwenyekiti watendaji wote ambao wapo maofisini kihasara hasara watakuwa na wakati mgumu zaidi.

“Mbali na hilo kwa sasa inaonesha wale watu ambao walikuwa wanapatiwa madaraka kwa njia ya kulindana itakuwa hadithi kwani waliowengi wanaweza kutimliwa,” kilisema chanzo hicho

Post a Comment

 
Top