Madiwani wa chama cha CUF waliofanya vurugu kwenye uchaguzi wa
Umeya katika Manispaa ya jijini Tanga ambao idadi yao ni
madiwani kumi
Kamanda Zubery Mwombeji alisema “kuwa madiwani hao walikamatwa
na kupelekwa katika kituo cha Polisi cha Chumbageni na baadaye waliachiwa kwa
dhamana majira ya saa sita usiku.
madiwani hao walikamatwa kwa tuhuma za kufanya vurugu na kuchoma
pazia na kujaribu kuvunja mlango wa ofisi ya Mkurugenzi wa halmashauri hiyo.”
Madiwani wa CUF wanadaiwa kufanya vurugu katika ukumbi wa
halmashauri ya jiji hilo uliotumika kupigia kura baada ya Mkurugenzi wa jiji
hilo kumtangaza diwani wa CCM, Mohamed Mustafa kuwa mshindi kwa kupata kura 19
dhidi ya mgombea wa CUF aliyepata kura 18.
CUF walipinga matokeo hayo na kudai kuwa walihujumiwa na kuporwa
ushindi hususan kwa kuwa wana idadi ya madiwani 20 dhidi ya madiwani 17 wa CCM.
Mimi nadhani cha
msingi wangeangalia wenyewe wote ni wasafi Madiwani wao au wapo waliokura
rushwa.
Post a Comment