Wawakilishi kutoka mabunge hasimu
nchini Libya wametia saini mkataba wa kuundwa kwa serikali ya umoja, kufuatia
mashauriano nchini
Morocco.
Mjumbe wa UN Martin Kobler akihutubia wajumbe kwenye mkutano huo
amesema leo ni “siku ya kihistoria kwa Libya”.
“Mchakato huu wa mazungumzo
umeonyesha kwamba Walibya wanaweza kutatua tofauti zao za kisiasa kupitia
mazungumzo ya Amani,” amesema.
Hata hivyo ametaja changamoto nne ambazo serikali mpya inafaa
kushughulikia, ambazo ni: mgogoro wa kibinadamu, mashauriano ya usalama wa
kitaifa, kukabiliana na kundi la Islamic State na makundi mengine ya kigaidi na
kuangazia Benghazi na maeneo mengine.
Akiandika kwenye Twitter, balozi wa Uingereza nchini Libya
amesema mkataba huo umepokelewa kwa shangwe na Walibya mjini Skhirat.
“Hii ni historia. Nimebahatika
kuishuhudia,” amesema.
Libya ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe baada ya
kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa muda mrefu Muammar Gaddafi mwaka 2011.
SOURCE BBC
Post a Comment