Mahakama Kuu Kanda ya Tabora inayosikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Kigoma Kusini iliyofunguliwa na David Kafulila dhidi ya washtakiwa; Husna Mwilima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya uvinza kama msimamizi wa uchaguzi na Mwanasheria mkuu wa Serikali ilipokea pingamizi toka kwa wakili wa Husna Mwilima kutaka Mahakama Kuu isiendelee na kesi hiyo kwakuwa Mhe Kafulila hakufuata taratibu katika ufunguzi wa kesi hiyo.
Katika utetezi wa mawakili wa Kafulila ambao ni Daniel Lumenyera naTundu Lissu waliomba mahakama itupilie mbali pingamizi hilo la wakili maarufu Fungamtama kwa hoja kuwa ni usumbufu kwa mteja wao na halina mana yoyote kwa kesi ya Msingi.
Jana Jaji anayesikiliza kesi hiyo Bi Leila Mgonya alizingatia ombi la Fungamtama na utetezi Lumenyela na kuamua kutupilia mbali pingamizi hilo la wakili wa Husna na kumtaka Husna Mwilima kumlipa Kafulila gharama za usumbufu kwa kuweka mapingamizi yenye sura ya kupoteza muda na usumbufu.
Aidha,Jana hiyo hiyo Mahakama iliendelea na hoja ya kutathmini gharama ya dhamana ambayo Mhe Kafulila atapaswa kuweka kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi iweze kuanza.
Uamuzi kuhusu kiasi gani Mhe Kafulila atalipa kama dhamana utatolewa leo na Mahakama.
Post a Comment