Historia, Sheria na Madai ya
Sheikh Ponda
 Na Ahmed Hussein          Â
Historia hukumbusha mbali sana. Historia hutia uchungu na hata kuliza kilio cha machozi! Kuna kisa cha Swahaba na Mwadhini maarufu, Bilal al-Rabaa ambaye wakati fulani, muda mrefu baada ya kutawafu Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, alizuru Madina akitokea Sham ambako alihamia.
Kwa mujibu wa kisa hicho, Bilal alipofika Madina alitoa ile adhana yake ya majonzi aliyokuwa akiitoa Enzi za Mtume. Adhana hii wangekuigia Masheikh wangu Abdallah Jafar, Ramadhani Mayumba na Mohammed Msoma, huenda ungepata majonzi hayo. Halafu, Bilal akazuru Kaburi la Mtume, ambapo kumbukumbu zikampelekea kulia sana!
Alilia kwa sababu alikumbuka historia. Alikumbuka enzi zile alizokuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Alikumbuka maisha yale yaliyojaa imani, huruma, ukarimu, uungwana, upendo, udugu wa kweli na kadhalika.
Kana kwamba picha nzima ya maisha yale ilimjia upya alipofika Madina! Kana kwamba picha ya Mtume ilimjia upya alipoliona kaburi lake! Kana kwamba alitamani zama zile zirudi tena! Bilal alilia kwa mengi kisha akaondoka moja kwa moja! Kana kwamba aliiaga Madina, âsasa kwa heri ya buriani!â
Huo ni mfano mmoja tu wa namna historia inavyoliza! Kwa ujumla, Historia ambayo sasa ni somo miongoni mwa masomo shuleni, hujaa kumbukumbu tamu na chungu. Uchungu wa Hadithi hutokana na ukweli kuwa baadhi ya kumbukumbu hujumuisha haki za watu zilizopotea kwa sababu za kihistoria.
Watu binafsi, familia, jamii, na hata Mataifa yamepata mkasa mmoja au mwingine wa kihistoria. Hebu Jamii ya Waislamu, mathalani, iitazame nchi kama Hispania na kisha ivute picha ya nyuma na kuiona nchi hiyo.
Hiyo ni picha ya enzi zake ilipokuwa chini ya dola ya Kiislamu. Leo hii huipati picha hiyo! Inapotajwa Hispania, mtu anaona labda ni Taifa lenye historia ya kijahili kama si kikafiri kabisa!
Muislamu wa Tanzania yeye anaweza kuvuta picha ya miaka ya mwanzoni mwa miaka 1960 hadi katikati yake. Katika kipindi hicho cha historia anaikuta Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki na miradi yake ya maendeleo pamoja na rasilimali ilizomiliki.
Ndipo anapokikuta kiwanja cha Changâombe. Historia, kwa uchungu, inamuonesha kuwa kiwanja hiki kilikuwa mali yenu. Hapo anatamani enzi zile zirudi tena ili kiwanja hicho kirudi tena mikononi mwa Waislamu kama jamii!
 Sio kiwanja cha Changâombe tu, zilikuwepo rasilimali nyingine nyingi sana. Historia, kama ilivyoandikwa na waandishi mashuhuri waadilifu hasahasa rafiki yangu Mhammed Said, ina hadithi ya kweli ya kutia simanzi kwamba mikono ya watawala ndiyo iliyowapora Waislamu rasilimali zao. Lengo lilikuwa ni kuwakwamisha wasifanye mengi ya kuendeleza jamii yao.
Mapambano ya âkufa na kuponaâ ya Sheikh Ponda Issa Ponda yaliyompelekea kuishia mikononi mwa Vyombo vya Usalama, vya Sheria na hatimaye kufungwa kifungo cha nje yaliakisi kumbukumbu hiyo ya historia. Ponda alisimama zaidi upande wa historia.
Ndiyo maana, mikono yake iliyokuwa ikifungwa pingu, ilikuwa ikikamatia kitabu cha Historia ya Mapambano ya Waislamu katika Harakati za kutafuta uhuru.
Ndani ya Kitabu hicho yameelezwa mengi mno ikiwa ni pamoja na jitihada za Waislamu za kujiletea maendeleo chini ya Jumuiya yao ya Afrika Mashariki au kwa kirefu chake cha Kiingereza East Africa Muslim Welfare Society-EAMWS.
Â
Jumuiya hiyo ilikuwa na mali nyingi mno ambazo ama zilitaifishwa na serikali au kumilikishwa kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania-BAKWATA baada ya Jumuiya hiyo kuvunjwa mwaka 1968.
Kisaikolojia, Ponda aliamini kuwa kushika kitabu kilichokusanya ushahidi wa maelezo ya kihistoria kungedhihirisha kile alichosimamia mahakamani. Kwamba yaliyoandikwa katika kitabu hicho kuhusu Kiwanja cha Changâombe ndiyo aliyoyasimamia.
Kwa bahati mbaya, ushahidi wa historia haukuwa na nafasi kubwa katika kesi hiyo kutokana na ukweli kuwa sheria ilisimama upande mwingine. Kwa falsafa yake, Sheria huhitaji zaidi vielelezo vya hatimiliki kuliko historia ya maelezo matupu.
Mbali ya Kitabu hicho cha historia, uthibitisho mwingine kwamba Ponda alisimama upande wa historia ni kule kuletwa Mahakamani Mzee Bilal Waikela wa Tabora ili awe shahidi wa upande wa washitakiwa. Sababu ni kwamba mzee huyu alikuwa miongoni mwa watu walioifahamu historia ya Jumuiya iliyovunjwa ya Waislamu.
Ni kweli, kama alivyosema shahidi huyo, Kiwanja alichodai Ponda kilikuwa ni mali ya Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki -EAWMS. Lakini kama tulivyoiona Hispania ambayo imebaki historia, rasilimali hizi, baada ya hujuma za mikono ya watawala, zimebaki historia.
Ukizidai kwa kutumia historia utaonekana âmkorofiâ tu, na sheria itakuandama! Hivyo ndivyo alivyoandamwa Sheikh Ponda. Ponda ameandamwa kwa sababu sheria, tofauti na historia, haikuwa upande wake.
Sheria hufuata mkondo wake bila kujali historia. Hata kama gogo limepatikana kwa njia za kijangili, msumeno hautajali hilo bali utafanya tu kazi yake. Msumeno hauwezi kugoma kukata gogo eti kwa kuwa halikupatikana kwa njia za halali.
Kwa kuzingatia fani zote mbili; ile ya historia na ile ya sheria, makala hii inataka kuzama kifalsafa ndani kabisa ya âjinaiâ iliyopelekea Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Ponda Issa Ponda, kuhukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja.
Nyuma hata kabla ya Ponda na wenziwe kufikiria kuingia Changâombe kwa madai ya kihistoria, kulishakuwa na watu mbalimbali waliokuwa wakizungumzia haja ya Waislamu kurejesha âmali zilizoporwaâ. Hawa nao pia walisimamia ushahidi huo huo wa kihistoria.
Hata kama Ponda, kwa wakati mmoja au mwingine, alipata kuzungumza na mmiliki wa moja ya vipande vya Kiwanja hicho chini ya kampuni yake ya Agritanza kuhusiana na madai ya Waislamu juu ya kiwanja hicho, basi kiini hasa si kingine bali ni historia ya kiwanja hicho.
Na hata kama kulikuwa na mapatano kuwa Kampuni hiyo iwape akina Ponda ekari 30 kama mbadala wa ekari nne za Kiwanja hicho, bado yote hayo yalizingatia ukweli uleule wa kihistoria kuhusu mali za iliyokuwa Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki.
Kwa msingi huo wa historia, Ponda na wenziwe walichukua hatua ya kijeshi ya kukamata kwa nguvu kiwanja hicho. Kama kulikuwa na jingine, Allahu aâlam-Ajuae Mola, mimi sina elimu ghaibu ya kujua undani wa nyoyo au nafsi za watu, bali nabaki ndani ya upeo wa falsafa ya historia.
Falsafa hiyo, pamoja na mambo mengine, inanisaidia kujenga hoja ya kuhalalisha dai langu kuwa historia ndiyo iliyowasukuma kina Ponda kuingia kijeshi Changâombe.
Kwamba mbona hawakuvamia uwanja wa jangwani ambao ni jirani na Msikiti wa Kichangani ambako Viongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu na wafuasi wao hupenda kukutana. Kwa hihi hawakuvamia viwanja vya Mwembe Yanga? Hawakuvamia viwanja vya jangwani na Mwembeyanga kwa sababu hawana historia navyo.
Kwa hiyo, tumeshajenga hoja isiyovunjika kuwa Ponda alisimama upande wa historia katika kesi iliyosababisha kifungo chake cha nje. Kwa mantiki hiyo, Kichwa cha Makala hii:Â âHistoria, Sheria na Madai ya Sheikh Pondaâ nacho kinapata uhalali.
Hata hivyo, kama nilivyodokeza katika utangulizi, vitu vingi vimepotea kwa sababu za kihistoria. Si kiwanja cha Changâombe tu bali majengo yamepotea kwa sababu hizo. Imebaki hadithi chungu tu ambayo vizazi vinapigiwa kwa mdomo au maandiko.
Hoja ya Ponda ingelikuwa na nguvu kubwa Mahakamani kama upande wake ungekuwa na kielelezo cha hatimiliki. Kwamba Mwanasheria wake angelikuwa na nguvu zaidi kama angewasilisha mahakamani kielelezo cha kuonesha hakimiliki ya kiwanja hicho chini ya EAMWS.
Kielelezo hicho kingesaidia kuhalalisha dai kuwa kiwanja husika kilikuwa na mgogoro. Si mgogoro wa kihistoria tu bali ni mgogoro wa kisheria. Hoja ya mgogoro ndiyo sasa ingehalalisha hatua zote za hapo kabla.
 Mosi, kuhamasisha Waislamu kuvamia Kiwanja, kuwazuia mafundi kuendelea na kazi ya ujenzi, na kupiga kambi ya kuhakikisha kuwa hakuna shughuli yoyote ya kuonesha kuwa kiwanja hicho kinamilikiwa na mtu.
Mbali ya hatua hiyo, pia, shauri lingefunguliwa mahakama ya ardhi kwa kutumia kielelezo hicho. Kwa wakati mmoja, kungelikuwa na kesi mbili. Kisutu jinai ya Ponda kuvamia kiwanja, na Mahakama ya Ardhi, âmadai ya Waislamu kuwa Kiwanja cha Changâombe kina Mgogoro.â
Upande wa Mashitaka ulioongozwa na Bw. Kweka ungelikuwa na wakati mgumu kama hatimiliki za EASMWS zingewasilishwa Mahakamani. Ni wazi mahakama ingekuwa na kazi ngumu ya kumthibitisha mmiliki halali kati ya EAMWS na BAKWATA. Na yumkini au bila shaka kabisa, kesi hiyo ingerejeshwa katika Mahakama ya Ardhi.
Lakini upande wa mwanasheria wa Washitakiwa ulipwaya kwa kukosekana kwa kielelezo cha aina hiyo. Alichobaki kukitegemea mwanasheria wa Washitakiwa ni jitihada tu za kuzuia ushahidi wa upande wa mashitaka. Kwamba mwansheria huyo alifanya kazi ya kujihami tu kisheria.
Ushindi wa mshitakiwa hutegemea mno uwezo wa kuvishambulia vielelezo au ushahidi wa upande wa mashitaka. Kwa jinsi sura ya kesi ilivyokuwa ni kwamba Upande wa Mashitaka uligawanya ushahidi katika makundi mawili.
Kundi la kwanza lilikuwa ni la ushahidi wa kufuta dai la mgogoro wa kiwanja. Na kundi la pili lilikuwa ni la ushahidi wa kuthibitisha uvamizi. Kwa upande wa kundi la kwanza, BAKWATA kama taasisi iliyomilikishwa Kiwanja baada ya kuvunjwa kwa Jumuiya ya EAMWS, ilikuwa na kazi ya kutoa ushahidi wa kwanza wa kuonesha kuwa dai la mgogoro wa kiwanja halikuwepo.
Kimsingi, mgogoro huo ungelikuwa ndani ya taasisi hiyo na si nje yake. Mtu angeweza kuuliza kwa nini BAKWATA ilianza na ushahidi wa kuimilikisha kiwanja Kampuni ya Agritanza, badala ya kuthibitisha kama kiwanja ni cha BARAZA hilo au Waislamu kwa ujumla?
Kwa sababu, hati za kiwanja zililipa Baraza hilo uhalali wa kumiliki, na tangu hapo, kuna tetesi kuwa Jumuiya ya awali haikuwa na hatimiliki, hati zilikuja kutengenezwa na BAKWATA. Shahidi wa kwanza wa BAKWATA akaanza na ushahidi kuwa vikao halali vilifanyika kuhalalisha hatua ya kuipa kiwanja kampuni ya Agritanza.
Hisia za awali za Waislamu zilituama katika dhana kuwa Kiwanja hicho kiliuzwa kwa kampuni hiyo. Jamii kubwa ya Waislamu iliamini hivyo. Na bila shaka Ponda na wenziwe waliamini hivyo.
Lakini shahidi wa BAKWATA akaondosha dhana hiyo kwa hoja kuwa Kiwanja hicho hakikuuzwa bali walibadilishana na kampuni hiyo, huku wao BAKWATA wakipata ekari takribani 40 za kutosha kuendeshea miradi mbalimbali hususan kujenga CHUO Kikuu.
Hoja hii ilileta tofauti ya hisia miongoni mwa Waislamu. Ikawagawanya kimaoni kwamba baadhi waliona kuwa kama ni hivyo, basi hakuna tatizo, na kizuri zaidi waliona maadam aliyemilikishwa ni Muislamu mwenye mapenzi na dini yake, basi yaishe!
Wengine wakaendelea na msimamo wa kutaka kiwanja cha Changâombe kibakie kama zamani kwani kiko mjini ambako thamani yake ni kubwa kuliko ekari 40 za Shambani.
 Kwa kiasi fulani, hoja hii ya BAKWATA ya kubadilishana kiwanja na Agritanza ilipoozesha dai kwamba kiwanja kiliuzwa. Hivyo, shahidi wa kwanza akathibitisha kuwa kiwanja hakikuwa na mgogoro wowote wa kimaamuzi ndani ya wigo wa BAKWATA.
Ilipotolewa hoja kuwa si Waislamu wote wanaoikubali BAKWATA, shahidi huyo alikuwa na kazi ndogo tu ya kujibu kuwa ni hiyari yao lakini taasisi inayomiliki kiwanja ni BAKWATA. Kimsingi, kama ni mgogoro basi ungepaswa kuwahusu wale waliondani ya BAKWATA na si nje.
Kwa kuwa ndani ya BAKWATA hakukuwa na mgogoro ndiyo sababu hoja ya walio nje ya BAKWATA kuwa kiwanja kina mgogoro haikuwa na nguvu za kisheria.
Watu waliozama katika fani za hoja za kisheria waliona umuhimu kwa Waislamu walioshitakiwa kujenga hoja kupitia kwa mwanasheria wao kuwa âBAKWATAâ ni Baraza la Waislamu wote. Hii si kwa maana kuwa wale wanaoipinga BAKWATA wamebadili msimamo, bali ni kwa maslahi ya kisheria.
Kama wangekubali hivi, basi hoja ya mwanasheria wa washitakiwa ingekuwa na nguvu, kwamba maamuzi ya kubadilishana Kiwanja na kampuni ya Agritanza yalifanyikaje bila Umma wa Waislamu wenye kiwanja chao kufahamishwa?
 Mwanasheria angekuwa na haki ya kudai BAKWATA itoe vielezo vya taarifa kwa Waislamu. Kwamba ni chombo gani cha Habari kilitumika kutoa âPress Releaseâ kwamba BAKWATA na KAMPUNI ya AGRITANZA zimebadilishana viwanja.
Kama BAKWATA ingeshindwa kutoa kielelezo cha Taarifa kwa Waislamu, sasa hoja ya kuvamia kiwanja ingekuwa na nguvu kwamba waliovamia kiwanja walifanya hivyo kuokoa mali yao waliyodhani imevamiwa kwani hawakuwa na taarifa kuwa yamefanyika mabadilishano.
Hapo pia hoja ya mgogoro wa kiwanja ingepata mashiko madhubuti kwamba maamuzi ya kubadili kiwanja hayakuwa na baraka za âWanabakwataâ wote kwa maana ya Waislamu kwa ujumla.
Kama ilivyokwishaelezwa, kwa maslahi ya kisheria, wote wangeikubali Bakwata, wasingikataa. Si kwa dhati ya kuikubali bali kwa ajili ya ushindi wa hoja za kisheria
Hata kama ingetolewa hoja kuwa âwao kina Ponda, mbona wana taasisi zao?â Bado neno âKuuâ katika jina la BAKWATA lingewahusu, kwamba sawa zipo taasisi nyingine lakini âBAKWATAâ ndiyo âkubwa yaoâ.
Izingatiwe tena kuwa hii ni hoja ya maslahi ya kisheria, si ya kuihalalisha Bakwata kwa wale wasioitaka. Hivi ndivyo unavyokuwa ujanja au kwa lugha nzuri zaidi tuseme âhekimaâ ya kujenga hoja za kisheria katika jitihada za kushinda kesi.
Ujanja au hekima hii ilikuwa muhimu kwa sababu upande wa washitakiwa haukuwa na hatimiliki. Laiti hatimiliki za Jumuiya ya Waislamu wa Afrika Mashariki zingekuwepo basi pasingelikuwa na haja ya kujenga hoja hii, badala yake hoja ya mgogoro ingejengwa kwa mgongano tu wa hatimiliki kati ya ile ya BAKWATA na ile ya EAMWS. Hapo ndipo wale wasioitaka BAKWATA wangekuwa na nguvu ya hoja.
Lakini msimamo wa kuisusa BAKWATA hata mbele ya Mahakama ulikuwa na maana ya kuzisusa mali zote zilizomilikishwa kwa Baraza hilo ikiwa ni pamoja na Kiwanja cha Changâombe. Hapo ndipo upande wa mashitaka ulipopata nguvu ya hoja, ânyinyi hamuitaki Bakwata, sasa kwa nini mmevamia kiwanja kinachomilikiwa na Baraza hilo?â

Post a Comment