Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
kimesema hakishtushwi kwani amekuwa akitumia hoja, mikakati na Ilani ya
Uchaguzi ya chama hicho.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu, amesema kuwa
wakati
wa kampeni Chadema ilieleza jinsi ya kupambana na ufisadi, kuwa na
utaratibu bora wa utendaji kazi, uadilifu na uzembe wa watumishi wa umma, mambo
ambayo sasa yanafanywa na Dk Magufuli.
Hata hivyo, alisema kwa kuwa anachofanya hakikuwamo katika
mipango ya Chama cha Mapinduzi (CCM), anaamini atakumbana na changamoto siku
zijazo.
“Akiomba ushauri tutatoa kwa maana namna gani atekeleze,
lakini ni mapema mno kusema kama ana dhamira ya kuyafanya. Pengine anayafanya
kwa ajili ya kujitafutia umaarufu wa harakaharaka,” alisema
Mwalimu.
Mikakati ya Dk Magufuli
Tangu Novemba 5 mpaka sasa, Dk Magufuli ametangaza mikakati
kadhaa ya kubana matumizi ya Serikali, ili kuimarisha huduma za jamii, sambamba
na kufichua na kuminya mianya ya rushwa na ufisadi.
Miongoni mwa mambo aliyoyafanya ni kusitisha safari za nje,
kupiga marufuku michango ya aina yoyote kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi
kidato cha nne, kufuta sherehe za Uhuru zilizotajwa kufanyika Desemba 9 na
kuagiza fedha za sherehe hizo zitumike kujenga barabara pamoja na kuibua madudu
ya ukwepaji wa kodi la rushwa katika Mamlaka ya Bandari (TPA) na Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA).
Mwalimu alisema mambo hayo ni kati ya mengi yaliyokuwa
yakipigiwa kelele na Chadema pamoja na vyama vilivyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa) kabla na wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba
25.
“Mambo haya (yanayotekelezwa na Dk Magufuli) tulikuwa
tumeyapeleka mbele ya Watanzania ili watuamini na tuwafanyie. Wananchi wanajua
nini kilichotokea na si ajabu kuona wao (Serikali iliyopo madarakani)
wanachukua ya kwetu na kuyafanyia kazi, maana Watanzania ndiyo walioyachagua na
ndiyo waliyokuwa wakiyataka,” alisema.
Huku akitolea mfano hoja za Chadema za ujenzi wa Chuo Kikuu
Dodoma (Udom) na kuandikwa kwa Katiba Mpya zilivyotekelezwa na Rais mstaafu
Jakaya Kikwete, Mwalimu alisema: “Uungwana ni vitendo (Dk Magufuli)
atakapokuwa anayafanya si vibaya akasema jamani haya yalikuwa si ya kwangu bali
nimeyakopa kutoka kwa wenzangu.”
Alisema si vibaya kwa kiongozi au chama kuiga mambo mazuri ya
chama kingine na kusisitiza kuwa lengo la upinzani ni kuona mambo ya msingi
yanafanyika ili nchi iwe na maendeleo.
“Suala atafanikiwa kwa kiwango gani hilo ni suala jingine,
kama anayafanya kwa utashi au kwa kuwahadaa Watanzania hilo ni suala
jingine.
Mwishowe kama si lako linakuwa na changamoto katika
kulitekeleza,”alieleza.
Alisema wapinzani hawawezi kuishiwa hoja za kuikosoa Serikali
ambazo nyingi zinalalamikiwa na wananchi, “Mambo yetu mengi
wameyachukua ila swali linakuja je, wanaweza kuyatekeleza? Chadema ni chama
chenye ubunifu wa hali ya juu katika kutafuta suluhu ya kero za wananchi.”
Alisema chama hicho sambamba na Umoja wa Katiba ya Wananchi
(Ukawa), wataendelea kuumiza vichwa ili kutafuta jinsi ya kuzitatua kero
zinazowakabili wananchi.
“Tunachokitaka kukiona ni Watanzania wakipata haki zao na
maendeleo, waishi katika nchi yenye demokrasia, utawala bora na misingi
mizuri ya sheria,” alisema Mwalimu.
Post a Comment