0
WIZARA ya mambo ya ndani ya nchi, imefuta vyama 1,268 vya  kijamii vya hiari vilivyopo Tanzania katika zoezi la uhakiki wa vyama hivyo. Vilivyosajiliwa ch
ini sura ya 337 ya sheria ya vyama 

Vyama hivyo vya hiari vinavyosajiriwa chini ya sheria ya vyama ni pamoja na taasisi za kidini.
Akizungumza leo na Waandishi leo msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya nchi, Isack Nantanga amesema kuwa  zoezi hili linalenga kufuta vyama ambavyo vimeshindwa kutekeleza masharti ya kisheria kuhusu kulipa ada za mwaka, kuhakikisha ukaguzi wa hesabu za chama na kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi.
Nantanga amesema kuwa zoezi la kufanya uhakiki liloanza mei mwaka huu limehusisha vyama 12,665 ambavyo vimesajiliwa katika daftari la msajiri wa vyama, wizara ya mambo ya ndani ya nchi ambapo 1,268 vimefutwa na 312 vimeridhia masharti ya mashirika yasiyi ya kiserikali chini ya sheria na. 24 ya 2002 inayosimamiwa na wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia na watoto.
Miongoni mwa vyama hivyo ni pamoja na Chama Cha Wahifadhi Mazingira na Usafi Pwani (HIMAUPWA ) Kibaha, Umoja wa Wanazuoni Tanzania, Rose Garden Social Club na Umoja wa Maendeleo ya Jimbo la Bumbuli.
Amesema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutiwa na baada ya siku 21 kuanzia leo, endapo vyama hivyo havitaonyesha sababu za msingi kwanini visifutwe, vyama hivyo navyo vitachukuliwa hatua ya vitafutwa
“Wizara ya mambo ya ndani inatoa angalizo kwa vyama vya vyote vya kijamii kuendesha shughuli zake kwa kufuata sheria na kanuni zilizowekwa na pia wizara itaendelea kuvifuta vyama vyote vinavyokiuka sheria hii,” amesema Nantanga.


Post a Comment

 
Top