Ingawa Rais Magufuli hajazitaja Wizara zitakazofyekwa, lakini habari toka serikalini zinasema kuna uwezekano mkubwa wizara zisizo na tija na zinazoweza kuunganishwa na kuwa idara chini ya wizara fulani, zikafyekwa.
Wizara hizo ni Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto ambayo huenda ikaingizwa kwenye ofisi ya Makamu wa Rais, hasa wakati huu ambapo ofisi hiyo inashikiliwa na mwanamke.
Nyingine ni wizara iliyokuwa ikishughulika na mambo ya utawala bora ambayo wadadisi wa masuala ya siasa wanapendekeza iwe chini ya Wizara ya mambo ya ndani pamoja na Takukuru ili kukabiliana na Rushwa.
Wizara ya Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira nayo inaweza kufyekwa na suala la Mazingira likasimamiwa na kila Wizara kwa kuwa na kitengo chake cha kusimamia mazingira badala ya kuwa na Waziri wake.
Wizara ya uwekezaji na uwezeshaji huenda ikafutwa na kuingizwa ndani ya kituo cha uwekezaji ( TIC ) na kuwa idara nyeti ya kusimamia maswala ya uwekezaji ikiwa chini ya wizara ya Viwanda na Biashara.
Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo nayo inapumulia mashine kwani huenda ikaungana na Idara ya Habari (Maelezo) na kuwa idara zilizo chini ya ofisi ya Waziri mkuu badala ya kuwa Wizara kamili
Wizara ya Kilimo na Mifugo inapendekezwa kuwa moja badala ya mbili kama ilivyosasa.Waziri katika ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) iliyokuwa inashikiliwa na Profesa Mwandosya yenyewe imekufa kifo cha Mende,kwani hakuna ubishi kwamba itafyekwa.
Post a Comment