Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta JOHN MAGUFULI anatarajiwa kwa mara ya kwanza kuwasili Makao Makuu ya nchi Mjini DODOMA kwa ziara rasmi ya kik
azi.
Katika ziara hiyo Rais MAGUFULI pamoja na mambo mengine anatarajiwa kuzindua Bunge la Kumi na Moja na kupendekeza jina la Waziri Mkuu wake.
Pia kikao hicho cha kwanza cha Bunge la Kumi na Moja kitapata nafasi ya kumchagua Spika wake mpya atakayesimamia shughuli za bunge kwa Miaka MITANO ijayo.
Keshokutwa siku ya Jumanne, Novemba 17 Bunge linatarajiwa kumchagua Spika, ambaye siku hiyo hiyo atafanya kazi ya kuwaapisha wabunge wa Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Alhamisi, Tarehe 19 Novemba, jina la Waziri Mkuu litawasilishwa kwenye Bunge ambapo ataidhinishwa na Bunge.
Siku hiyo hiyo Bunge litafanya Uchaguzi wa naibu Spika.
Post a Comment