Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kahama, James Lembeli ameelezea kinachoendelea katika maisha yake ya kisiasa hasa baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka huu akiwa ndani ya chama chake kipya cha Chadema.
Akiongea katika taarifa rasmi kwa wananchi wa jimbo hilo, Lembeli amesema kuwa hivi sasa atajikita zaidi katika shughuli za chama chake pamoja na shughuli alizokuwa akizifanya
kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.
kabla ya kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Alisema kuwa ataendelea kufanya kazi zake na mashirika ya kimataifa kama mjumbe wa Bodi mbalimbali. Pia, ataendelea kufanya kazi ya kusimamia radio yake (Kahama FM) ambayo amedai kuwa taarifa zilizosambazwa kuwa ameiuza kulipa deni la mkopo aliopewa kuendesha kampeni sio za kweli.
Pia, Lembeli amewashukuru wananchi waliojitokeza kumuunga mkono na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika masuala ya maendeleo na ataendeelea kushirikiana nao kukamilisha miradi mbalimbali aliyokuwa ameanza kuitekeleza kwa juhudi zake binafsi.
Kadhalika, Lembeli amekanusha taarifa zilizokuwa zimesambazwa kuwa alikamatwa na jeshi la polisi mara tu baada ya Jumanne Kishimba wa CCM kutangazwa kuwa mshindi.
Post a Comment