0

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Tarime Mjini, Mwanjombe limemtajngaza rasmi Ester Matiko (Chadema) kuwa mshindi katika kinyang’anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.
 
Matiko amekuwa mbunge wa kwanza kutangazwa rasmi huku akiweka histori kubwa katika wilaya ya Tarime mjini kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mbunge katika wilaya hiyo inayosadikika kuwa na historia ya mfumo dume hususan katika ngazi ya familia.
 
Bi. Matiku  amepata kura 20,017 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Kembaki Michael Mwita wa CCM aliyepata kura 14,025

Jimbo la Siha
Ubunge: Dk Godwin Mollel (Chadema) 22,746 na Aggrey Mwanry (CCM) 18,584.
 
Msimamizi wa Uchaguzi, Rashid Kitambulio amemtangaza Dk Mollel kuwa mshindi wa jimbo hilo ambalo mbunge wake alikuwa ni Aggrey Mwanry (CCM).
 
Jimbo la Tunduma
Ubunge: Mwakajoka Frank (Chadema) 32,442, Frank Sichalwe (CCM) 17,220, James Mwakalonge(TLP) 85, Reddy Makuba (ACT Wazalendo) , 319.
  
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Tunduma, Halima Mpita ametangaza matokeo hayo.

Post a Comment

 
Top