0

Tukiwa bado tupo kwenye headlines za Uchaguzi 2015 hivi karibuni kumekuwa na taarifa zilizoenea kuhusu vijana waliopatikana katika mikoa kadhaa kusimamia kura au masanduku ya Uchaguzi Mkuu
2015 katika kila jimbo.
 Emmanuel Kawishe mwanasheria wa tume ya uchaguzi amesema .’Hakuna watu walioteuliwa kwenda kusimamia masanduku na tume itaanza rasmi kuwateuwa kuanzia tarehe 26 mwezi wa tisa sasa hivi tume imeanza mafunzo mpaka tarehe 3 mwezi wa kumi tunatoa mafunzo kwa usimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo na wasaidizi wao tutaenda kwenye kata pia  tutaenda kwenye vituo kwa hiyo hao ndio tume itatoa mafunzo kwao  – 
‘Sheria inakataza kwamba haruhusiwa mtu yoyote kupiga kampeni siku ya uchaguzi wala haruhusiwa mtu kuja na nguo ya chama chochote katika chumba cha kupigia kura kwa hiyo  wewe njoo na nguo za kawaida na kadi yako ya kupigia kura basi wasimamizi watakupa maelekezo ya kila kitu‘ 

Post a Comment

 
Top