0
Mgombea wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli amesema iwapo atapewa ridhaa ya kuingia Ikulu atapambana kuhakikisha Watanzania wengi wanapata ajira na kwamba anakerwa sana na kigezo cha mtu kuwa na uzoefu ndio apatiwe ajira.

Dk Magufuli alienda mbali na kusema kuwa kama kuna uwezekano, kipengele hicho kinachowataka watu kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa kama kigezo cha kuajiriwa huku akitoa mifano ya watu wanaaomba nafasi mbalimbali za uongozi wa kisiasa akiwepo yeye mwenyewe kuwa hawana uzoefu wa nafasi hizo lakini wana uwezo wa kuongoza.

Katika kampeni zake mjini Iringa jana, Magufuli pia aliahidi kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda mjini humo ili kupunguza tatizo la ajira kwa vijana.

Alisema kuwa wapo vijana wengi wanaohangaika kupata ajira baada ya kuhitimu kwa kuwa ajira nyingi zinahitaji watu wenye uzoefu wa kufanya kazi hivyo inakuwa kikwazo kikubwa kwa wahitimu kupata nafasi hizo.

‘’Vijana wengi wanaomaliza vyuo mbalimbali wanapatashida kupata ajira kutokana na waajiri kuhitaji uzoefu, sasa mwanafunzi ambaye amemaliza chuo leo atapata wapi uzoefu wakati hajaajiriwa?.. tena wanataka uzoefu wa miaka mitano huo uzoefu wataupata wapi, nataka kama kuna uwezekano haya mambo ya uzoefu yafutwe kabisa,” Dk magufuli.

Alieleza kuwa serikali yake itajikita katika ujenzi wa viwanda ili kumaliza tatizo hilo sugu kwa wananchi wa Iringa na Watanzania kwa ujumla. 

Aliwataka wawezekaji wenye uwezo wajenge viwanda mkoani Iringa ili Watanzania wanaomaliza vyuo vikuuu waweze kupata ajira.

Post a Comment

 
Top