Mbeya ambayo naambiwa Jeshi la Polisi Mbeya wamekataza maandamano ya Chadema ambao yalikua yafanyike Aug 14 wakati wa kwenda kumpokea Mwanachama mpya na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowasa.
Barua ya Jeshi la Polisi ambayo imetolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi,Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Mbeya Ahmed Z.Msangi ikikataza maandamano hayo na kukubali kufanyika kwa mkutano tu
Tangazo kwa umma.
Mnamo tarehe 10/08/2015 ofisi ya mkuu wa polisi wilaya ya mbeya ilipokea barua toka chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) inayohusu taarifa ya mkutano wa hadhara utakaofanyika tarehe 14/08/2015 katika viwanja vya ruanda nzovwe.lengo la mkutano huo ni mgombea wa raisi kuomba wadhamini
Leo tarehe 13/08/2015 jeshi la polisi mkoa wa mbeya lilikutana na uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo akiwemo mbunge wa mbeya mjini na baadhi ya madiwani katika eneo la usalama wa chama hicho katika ofisi ya kamanda wa polisi mkoa wa mbeya na kufanya mazungumzo kisha kufikia makubaliano kama walivyotoa taarifa yao kuwa hakutakuwa na maandamano bali ni mkutano. Hii inatokana na;
- Sababu za kiusalama
- Kutozuia watumiaji wengine wa barabara hiyo ikizingatiwa barabara kuu itakayotumika ni moja.
Hivyo basi kamanda wa polisi mkoa wa mbeya anatoa rai kwa wananchi kutofanya au kulazimisha maandamano yoyote yawe ya miguu au pikipiki.hii ieleweke kwamba si maandamano bali ni mkutano wa hadhara utakaofanyika katika viwanja hivyo. Kinyume na hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Pamoja na hiyo pia nilifanikiwa kupata mahojiano ambayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya alifanya na kituo cha Radio cha Bomba Fm kwenye kipindi cha Bomba Base Show,unaweza kubonyeza play kusikiliza.
Post a Comment