0

Sehemu ya 3


Mtunzi.  Long live josephat

Ilipoishia toleo lilopita, habiba anamdadisi james kuhusu kevi, baada ya james kumwambia kua anamfahamu kevi na kwamba kevi anasifa mbaya, habiba anatamani kujua sifa za kevi lakini, ghafla gari inatokea james anapanda na kumua
cha habiba akiwa na maswali mengi kichwani, habiba anampigia simu james ili kumdadisi tena hatimaye james anam
wambia habiba siri nzito inayomkatisha tamaa ya maisha, habiba anagundua kua kevi ni mchafuzi wa wanawake na anaweza akatembea na wanawake wote nyumba moja ili mradi tuu ausambaze ukimwi na awapige picha za utupu kwa maslahi yake binafsi, habiba anakata simu kisha anajilaza kitandani akiwa hana lakufanya,  songa nayooo......." Habiba, habiba ,habiba"... niliskia sauti ya dada yangu aliyekua akinishtua sikujali sana lakini aliniambia niamke chai teyari..." kwani saa ngapi saizi"...niliuliza ili niwe na uhakika zaidi.." saa tatu asubuhi"... batuli hakunielewa alihisi kama sipo sawa alinitwanga swali.. " vipi kwanii?"....nilijibu kwa hofu kidogo.."hamna nilikua naota ndoto mbaya sana"..." inahusu nini hiyo ndoto"...batuli aliuliza kwa haraka huku akiwa ananidadisi kwa makini sana.."aaah nilikua naota nakimbizwa na watu hata siwajui"...."acha mawazo yako amka ukanywe chai".. nilimtoka kwa stahili ile maanake ningemwambia ukweli ingekua balaa, kusema ukweli nilikua nashindwa kutofautisha ni ndoto ama kweli maskini mimi Habiba naenda kuchanganyikiwa sasa, nilichofahamu mimi ni kwamba nina ukimwi na picha zangu sijui nani ameziona mpaka sasa yote hayo kwa ajili ya kevi, ndiooo! sikua na uhakika kama nilikua naota au lah, hivyo ilibidi niende kwenye simu yangu maana nakumbuka niliongea nasimu jana, nilipoiangalia simu yangu nilikuta missd call kama kumi. Hivi zilikua za james na mesej kama mbili, hivi, zote zilikua za james,, " mungu wangu kumbe kweli nilikua naongea na james"..njlijikuta nikijisemea kimoyo moyo sikua na jinsi, ikabidi nianze kuamini kua si ndoto tena bali ni kweli, nilifungua zile mesej kuona zilikua zinasemaje,,meseji ya kwanza ilikua inasema kama ifuatavyo..."  vip mbona hupokei simu?"  Meseji ya pili ndio ilionichanganya kabisa nakunifanya nianze kulia..." daaa yule jamaa inasemekana akikuacha ujue anauhakika kua kakuambukiza na picha kaziweka teyari mitandaoni kuna gazeti la ijumaa la jana naskia kunapicha kibao za hao madem ambao kevi kawapiga picha na kawaweka wakiwa uchi. Jamaa wangu analo kasema, nitakuletea kama unahitaji kuhakiki ninayo sema"...kwakweli ukisikia kufa ndio huku, sikua na hamu ya chai wala kitafunwa cha kwanza kabla sijajiua niliandika meseji kwenda kwa james....akhasante mpenzi haina haja achana nalo tuu"....nilimjibu ili asilione lile gazeti ingekua aibu kama angeiona picha yangu kwenye lile gazeti sikutaka yawe makubwa sana"..nilichofanya ni kujitanda baibui na kutoka nje bila kumsemesha mtu nilienda mpaka kwa muuza magazeti. Sehemu wanayouzia sio mbali na nyumbani hivyo nilienda haraka,,jamani nyie acheni nilikua najikaza tuu maanake nilikua mzima usoni ila nilikua maiti moyoni,..." mambooo"...nilimsalimia yule muuza magazeti sikujali salamu yake au anirudishie salamu..." gazeti la ijumaa la jana lipoo"?...yule kaka alinichomolea gazeti hilo alilokuwa kaliweka. Chini yamifuko yake mikubwa ya kubebea magazeti,,nilimpa elfu moja kisha nikaondoka zangu bila kujali chenji,,upesi upesi mpaka chumbani kwenda kuangalia ni nini kimo ndani,, juu kabisa ukurasa wa mbele palikua pameandikwa, kwa herufi kubwa..."UFUSKA WAENEA TZ"...hapo nikatekwa na kichwa cha habari nilipo endelea kusoma zaidi nikaiona picha ya Kevi pembeni yake kukiwa na habari inayosema..." Tazama mabinti 60 walio pigwa picha za utupu na bwanawao mmoja"...ile habari ilikua ukurasa wa pili,, sikuchelewa moja kwa moja mpaka ukurasa wapili,, kwakweli zile picha zinatisha. Nyie kevi ni mnyama muuaji kabisa,,basi nikaanza kuperuzi picha moja moja,, ndipo nilipo toa macho na kushangaa kukuta picha ya mwanamke flani ambaye nilimkuta na kevi na kumuambia kevi achague kati ya yule mwanamke au mimi,, picha ilikua ni ya utupu na aibu yule mdada alikua uchi japo kwenye gazeti walikua wameziba waliweka doti jeusi ili mtu asione sehenu za siri,," mungu wangu"... nikijikuta nikijisemea mwenyewe, nikaendelea kuperuzi nikaikuta picha ya mwalimu wangu wasekondari,,nikawa nashangaa tuu, baadae nikaikuta picha yangu,, nguvu zote ziliniiisha,,"daaah amakweli kevi kaniweza",, nilijisemea moyoni, ilikua ni picha ninayoikumbuka tena ilikua ni siku ambayo bibi alipelekwa muhimbili kwa ajili ya matibabu ya ugonjwa wake wa kisukari,,nakumbuka nilidanganya naenda kwa shangazi, kumbe wapi nikapitia mojamoja mpaka sinza kumekucha kwenye gesti alio nielekeza kevi kua tukutane,  nililia kwa uchungu kisha nikanyamaza,,bahati nzuri ile picha ilikua hainionyeshi sura kwa sana nilikua kama nakataa kupigwa ile picha nikajiziba uso kidogo hivyo haikuweza kunitoa uso mzima,, ila kwa mtu wakaribu akiangalia kwamakini ni lazma anijue kwakua ilikua imetoka vile sio mbaya nikashukuru pia,, tatizo ni jee vipi akiamua kuzitoa na nyingine itakuaje?, basi sikua najinsi ilibidi nilifiche lile gazet, asijue mtu yeyote juu ya yale mambo,,wakati natafakari hayo nikakumbuka suala la ukimwi swala ambalo lilinifanya nitafute glass moja ya maji na sumu kidogo ilikua sumu ya panya,,nilimimina kisha nikaiweka kando kidogo,,nikatoka nje kwenda kumuaga baba nilikua nataka kujiua kwa staili ya aina yake nilimuaga baba kama natoka ivi na nikamuaga mama mkubwa na batuli pia,nilitaka wajue nawapenda hata nikifa wajue nilikua nawapenda,nilikua nimeiandaa nakaratasi yangu yakujiua yaani kama nimeacha waraka flani hivi,,chakushangaza na chakutisha nilipoingia chumbani nilikuta mtoto. Mdogo wa anti yangu ana umri wa miaka kama mitano akiwa analia kwa uchungu na ile glass yangu ya sumu nikawa siioni tena pale nilipo iweka,,nilipiga kelele za ajabu sana,, nikawa nalia sana,, huku nikisema nimeua nimeua,, nimeua,, yaani mawazo yangu na fikra zangu zikawa zimehama kabisa kwangu nikawa nalalamika juu ya uamuzi nilioufanya wakuweka sumu kwenye glasi na kuiacha,, ile sumu ilikua inakama weupe flani wamaziwa nilipoichanganya na maji kidooogo,, nilijua fika Deusi, atakua kainywa ile sumu kwa sababu Deusi anatabia ya kupenda sana kula au kunywa vitu vilivyoachwa na watu na nikizingatia ule weupe alijua ni maziwa ,,sikua na jinsi nilibaki nalia mpaka hapo nilipopoteza fahamu kwa kujua nimeua mtoto washangazi,,baada ya muda nilizinduka nikiwa kitandani nilikua sijielewi kidogo, nilipoamua kwenda nje kutoka kuuliza juu ya mimi kudondoka nikakumbuka juu ya mtoto wa shangazi tumbo likaanza kuniuma, nilienda jikoni nikamkuta mamkubwa anaosha vyombo kwakweli niliogopa sana nikauliza kwa kudadisi...."mamkubwa eti umemuona Deo"...mamkubwa hakunijibu nilitaka nishtuke ila ndani ya sekunde alipaza sauti..."Deoooo. Njoo unaitwa na Dada yako".....Duuu huwezi j
Amini jinsi nilivyofarijika kuskia vile maana nilichokua nahisi ni kikubwa sana nilikua nahisi Deo amefariki kwa ile sumu nilioiweka kwenye glass...baada ya dakika moja deo alikua amefika..." Naaam"..deo aliitika ili apewe tena maelekezo kua kaitiwa nini..."dada yako anataka aongee na wewe"...mamkubwa alisistiza, basi nilimchukua Deo nikaenda nae mpaka chumbani kwangu nikawa na mdadisi kama alikua amekunywa ile glass ya maziwa lakini niligundua kua hakunywa kwasababu kwa spidi ya ile sumu asingeweza kupona ingekua kwa heri,, nilimpa shilingi miatano akanunue pipi kama kuzuga tu ili nimtoe mchezoni,alipoondoka likaja wazo kichwani mwangu lililokua linaniambia kua nisisahau kua ninaukimwi,,niliogopa sana nililiendea lile gazeti nikakuta halipo ile sehemu nilipo liweka nikasaka sana mule ndani bila mafanikio lakini wapi!! nilipotoka kwenda kumuuliza mamkubwa nilimkuta baba sebuleni kakaa analisoma lile gazeti nilitamani nimpokonye lakini sasa nitaanzaje na analomkononi kevi mzee anamfahamu lakini sio sana alishawai kuniona nae siku moja kwahio kama angemuona angejaji au angeniuliza,, wakati najiuliza yote hayo baba aliniita kwa ukali sana..."wewe hebu njoo hapa".."mungu wangu mtumee atakua kaiona ile picha yangu au kamuona kevi mama yangu nakufa leo"...nililia kimoyo moyo lakini nilijikaza nilimfuata ili nimsikilize anasemaje..." ivi wewe unamatatizo gani ni wanaume au uwehu wako ndio unatupa shida sisi hapa nyumbani mbona hatukuelewi juzi umekunywa sumu mara ukawa unalia, leo umezimia.,Tatizo ni nini hasa hebu tuambie"..." hamna tatizo baba" ...nilijibu kwa uwepesi lakini alijua kua tatizo lipo,," sasa basi kama hamna tatizo staki kuskia tena huo upuuzi wako na shule zipo karibu kufunguliwa na chuo ulichoomba nimeshakufanyia mpango pale mwezi wakumi utaanza hapo mwalimu nyerere kigamboni. Sawaaa"... alimalizia kwa msistizo kidogo lakini nilimuelewa,,sikumjali nilirudi upesi chumbani kwangu japo sikufanikiwa kuondoka na gazeti lakini nilishukuru kwa jinsi nilivyochomoka pale,,basi nikawa sina hili wala lile,, nikawa njia panda nikaamua,,nipange safari yakutoroka kwenda mkoani maana nilikua nataka aibu inikutie mbali sio pale nyumbani ukizingatia mazoezi ya kutaka kujiua yameshindikana, nilipanga nguo zangu vizuri nikaanza kuiwaza safari ya kutoroka nyumbani, ikua niondoke na fedha kidogo lakini niliona nichukue na pete na vitu vingine vya thamani kama vile pete za mama mdogo na vito vya thamani ili niuze mbeleni nikikwama kifedha,,basi nikawa nimepanga hivyo,,wakati nawaza yote hayo kunasimu iliingia nilipoipokea nikakuta miss call nilipo piga ikapokelewa na jamaa mmoja aliekua  yupo makini na hapendi longo longo kwa jins sauti yake ilivyokua inaskika pamoja na uongeaji wake.." halow"...niliita kwenye simu,"..hallow samahani naomba kesho saatano tukutane magomeni nina habari ambayo inakuhusu sana fika bila kukosa na usije ukajutia baadae"....kisha simu ikakatwa nilipiga mimi ila kakata yeye,, niliduwaaa kidogo lakini sikukubali nikampigaia tena simu akawa hapatikani,, nilijiuliza sana ni nini tatizo au kuna ugomvi kunakitu cha kubadilisha maisha yangu zaidi yakupona ukimwi, kwakweli hapana huyu sijui ni nani. Anataka nini,,aaah siku mjali niliendelea na mipango yangu,

Fuatilia bila kukosa jeee nani alepiga simu na je habiba atafanikiwa kutoroka
Habiba atakubali wito

Fuatiliaaa hapa hapa



Sehemu ya 4


Ilipoishia toleo lililopita, " Habiba anachanganyikiwa baada yakupoteza dira ya maisha, kwa skendo na ugonjwa wa ukimwi anaoamini kua kevi ndio kamuambkiza, anapanga kutoroka kwao, ili aende kusiko julikana kwa jili ya kukwepa aibu na lawama, wakati yupo kwenye harakati hizo za kutaka kutoroka ghafla anapokea simu, na anapewa masharti kuwa wakutane magomeni saa tano asubuhi, na asijaribu kutokufika kwani atakuja kujutia, habiba haelewi ni nani anaongea nae wala kwanini kapewa ujumbe ule, anakua njia panda na haelewi la kufanya, anajikaza kwa kufanya maamuzi ya kuendelea kutaka kutoroka. Songa. Nayooo....." Aaah. Da kwani nimekosa nini mimi?,sijui nimekosea wapi maskini mbona mungu ananiadhibu, namna hii sina tabia ya umalaya lakini sasa naonekana malaya tena mwenye ukimwi tena nayetokea magazetini, ama kweli hujafa hujaumbika".....nilijisemea moyoni kwa uchungu sana, nilikua nimeanza kupaki mizigo yangu lakini niliacha kidogo nikaanza kuitafakari ile simu, sijui atakua mshenzi gani huyu aliepiga simu alafu eti anadai nikutane nae magomeni nisipoenda nitajutia, huyu jamaa fala kweli sijui vipi kwanza simjui alafuuuu"  ......"  nilisita kidogo nikajisemea kwa sauti ya chini chini ya kujutia kidogo"......."mamaaaaaaaaa. Mungu wangu sio kevi huyu ndio amepiga simu, daa sijui itakuaje anataka nini tena kwangu au kuna ishu imetokea tena?,  ngoja,  lakini mbona sio sauti yake kabisa,, .ngoja nimuulize James pengine atakua anajua yule mbwa anakaa wapi, maana huku mwananyamala simuoni sikuizi nahisi kahama, ,lakini james atakua anajua yupo wapi au anakaa wapi ngoja ni mdadisi kidogo"......"nilijikuta naongea mwenyewe nikiwa najiuliza nakujijibu mweywe ukiwa kwenye hali kama yangu, ngoja nikwambie, hupati, usingizi, huogi ukatakata, hupati hamu ya kula, kila mtu kwako ni adui, nakikubwa uoga na kuwaza kifo kila mara bila kusahau,hamu ya mapenzi inakua imekufa yaani kama mwanaume upo kwenye hali kama yangu, hata iyo mashine yako kusimama tena sahauu, nyie acheni tuu, sikia tu kua mtu anaukimwi ,, basi niliinyanyua simu yangu nikampigia james, ilikua usiku mida ya saa tatu ivi, james aliipokea simu yangu,, kiukweli jamani james simkubali kabisa yaani basi tu sijui nilikua nawaza nini, lakini sikutaka iwe topic kwasababu ndo nishaharibu tena basi mazungumzo yakawa hivi",,,,Habiba..."mambooo"......james "..poa tu mpenzi mambooo".....habiba ......"nimekumiss ile mbaya uko wapi baby"....james......." nipokitandani nakuwaza wewe"......"aaah yaani james alikua anajaribu kuleta hisia kwangu yaani angejua mwenzake waala hata sijali, mi nia yangu tuu, nikutaka kujua yule mpumbavu kevi anakaa wapi nipate uhakika kama ni magomeni au lah,"  habiba....."  kweli mpenzi, unaniwaza mimi".?.....james...." haswaaa baby wangu wa dhati"....." wanaume waongo nyie sikutaka kujaji saaana nikaingia kwenye dhumuni"........."eti baby yuleeee, yuleee, naniiii, kevi.  Nimemuona mitaa yetu tena, hivi anakaa wapi au ndio anausambaza ukimwi wake na huku kwetu"...."niliuliza swali kwa kujifanya namchukia kevi,nikweli namchukia lakini nilizuga chuki nilizipeleka kwenye kudadisi zaidi"..........james...." yaaaaa,  yule jamaa kweli anaitwa kevi anakaa mwananyamala kwa mama zakalia, sasa ivi,, vipi umemjuaje jina baby"?......" james alinipiga swali ambalo sikutegemea nilichekecha kichwa upesiii nikajibu ,mwanamke , uongo hua haupotei kwangu,"....habiba....." anhaaaa nimeliona lile gazeti la ijumaa bwana si ndio kusoma ndani nikaiona picha yake na jina, kwaio ndio nikamjua jina gazetini".." mwanamke nikamaliza zoezi na swali gumu kwa jibu jepesi sana" ........james....." sawasawa. Basi ndio ivyo bwana yule jamaa apana chezea weka mbali na watoto ni silent killer kesha ua kibao nawengine anawatesa vitandani"....."daa yaani yale maneno yake james yalinikata maini sikua nahamu tena yakuongea nae, nilimjibu kua simu yangu haina chaji bettry low inakata sasa ivi,kwaio nilimuahidi nitampigia ikijaa chaji"......" shenzi kabisa utasubiri mpaka ukome sipigi tena simu" ..."nilisema kwa hasira sana,nikiwa chumbani kwangu"  ...." hapo sasa nikawa nina mtihani tena sasa yule alie nipigia simu ni nani kama sio kevi?, aah nikaamua kuvunja ukimya nikamtumia meseji,, niliogopa kumpigia sauti yake unatisha alafu yupo serious sana, nikamtumia sms" ....." vipi we nani mwenzangu sikupati vizuri, sina namba yako alafu umesema tukutane magomeni kuna nini,?, nikaituma punde tu baada ya kumaliza, hazikupita dakika akatuma na yeye sms yake ilikua kama ifuatavyo,"  ....." wewe ukifika magomeni saa tano utapata majibu yote hayo"......"duu huyu mtu ni jambazi au? mbona hivi tena, basi sikutaka kujifanya najua sana maana nilijifanya najua kupenda nikaumbuka,, ngoja tu kesho ifike nikakutane naye huyu mpuuzi sijui kuna nini" ....." usingizi unakuja basiiiii!! mbwembwe tuu yaani full kuesabu nondo, daa we acha tuu",......kesho yake mungu akajaalia ikafika sina tena u sister duu nilikua nimeshapagawa yaani basi tu no saloon. No kula kula, yaani mungu huyu kwakweli yeye pekee ndio anajua navyoteseka, nilijiandaa haraka haraka, nikawa napita sitting room, ghafla baba akaniita, nilitukana kimoyo moyo, siwez sema ni tusi gani,," "daa huyu naye anataka nini sijui"..."nilijikuta na mzalau baba yangu mzazi ila sikujali mimi ndio nilikua mtu mwenye matatizo makubwa kuliko yeye anayelisha familia kwaio sikujali kabisaa."..
......baba....."habiba vipi wapi tena".?..
..."aliuliza ikabidi nijibu tuu kwa kuongopa ndio maisha yangu hayo ya kila siku ukweli nausema moyoni mdomoni uongo tupu"...
."natoka naenda kwa rafiki yangu"....."nilijibu kwa ufupi tuu".....
...baba.....".mbona mapema sanaaa?" ....
" daa yaani angejua ananichelewesha kuwahi magomeni na kifoleni hiki cha asubuhi asinge thubutu kunigasi".
....habiba...."kuna kazi naenda kumsaidia rafiki yangu"....
..baba....." sasa mwanangu kunasehemu nataka twende sio mbali sana ila naahidi kukuwahisha kwa huyo rafiki yako sitokuchelewesha," .

..." .daa huyu mzee hajui alitendalo, nilimalizia neno langu la moyoni nilimkubalia kwa kichwa"......" kumbe alikua kesha waambia na wakina batuli kuwa leo tunatoka nikamuona mamkubwa na Batuli nao wamevaa safi wanakuja tulipo mimi n! Baba,"...
...baba...." haya twendeni tuwahi jamani".....
." sijui tunaenda api au shamba maana asije akafanya nichelewe huyu kwa yule jamaa Wa magomeni" nilijisemea moyoni kama kawaida yangu"....
 ...baba......"haya tumefika jamani" ......"baba alituambia tushuke kwenye gari tumfuate sikujua ni wapi tunaelekea lakini nikama kwenye hospitali iv ila sikujali wala nini, nilijua kutakua kuna mgonjwa amekuja kumuangalia,, mara tukakaa kwenye benchi lile la wagonjwa sikumuelewa baba ni nini kimetuleta na hamna alieuliza kitu kila mtu alikua anangoja kuona nini kinaendelea ghafla alikuja nesi akamchukua baba na kwenda nae mpaka chumba flani sikujali pia,, baada ya muda kama dakika kumi na tano mzee alitoka akiwa ameshikilia kapamba kadogo mkononi juu kidogo ya paja la mkono, nikama alikua kaenda kutoa damu hivi,ghafla alikuja tena yule nessi,  akaja kumchukua Batuli, nae vile vile akaja kama baba na pamba yake akiwa anaskia viuchungu kidogo vya kutobolewa,wakati nashangaa yote hayo ikabidi nimuulize mzee"  ......"baba vipi mnaumwa au mbona mmeenda we na batuli kutoa damu"..." mzee kabla hajajibu alikuja tena yule nessi kisha akaniamuru nimfuate nikamuangalia baba ,baba nae akanipa ishara kua niende naye basi nikamfuata, kufika kule nikakutana na dokta akaanza kupiga stori na mimi  sikuelewa kamchezo kanaendaje ghafla nikaanza kuambiwa, sijui nisihofu nivizuri nimekuja kuangalia afya yangu na kwamba. Vipimo vitakua siri kati yangu na yeye,"
     "mungu wangu leo nimekamatwa mkojo ukaanza kubana haja pia ikaanza kubana,yaani kumbe mbwembwe zote zile kumbe ni kupima ukimwiiiiii, leo naumbuka mimi,  habiba yamenikuta"
 ...."nyie acheni tuu nilianza kulia pale pale tena kwa nguvu,, dokta akanibembeleza kisha wakaanza kunihoji maswali yao, niliongopa kila kitu kisha nikaomba ruksa yakwenda chooni walikua wamesha aanza kunitoa damu yule dokta baada yakumaliza , aliniruhusu niende cbooni kisha nirudi kuchukua majibu yangu,",
" nani wakurudi labda sio mimi na hii ndio tiketi yakuondokea nakutoroka sina tena mpango wakubaki"....kimoyo moyo nilitamka huku nikiwa natoka mule ndani kwa dokta, nilitafuta mlango wapili wakutokea kisha nikaanza kuondoka zangu kuelekea nyumbani waache wasubiri ila mimi sipo tena dar es salaam hii, nilirudi kuchukua begi langu languo kisha nikaanza safari yakwenda kwanza magomeni,  nyumbani alikua kabaki mfanyakazi tuuu ,alikua yupo na mtoto,, sikumjali na hakuuliza kwanini nimerudi peke yangu, nilichukua kila kilicho changu nachoweza kubeba nikatimua mbio, pesa nilikua nayo ya nauli na matumizi ilikua kama laki mbili na nusu hivi ,baba alinipa nikanunue simu lakini sikununua nilikua nina mipango nayo mingine kabisaaa, nikachukua gari za kariakoo kwakua nilitokea nyumbani, basi mojakwa moja ikaanza safari ya magomeni, bahati nzuri foleni ilikua sio kubwa sana hivyo nikawai kufika pale magomeni, niliposhuka tuu nikampigia jamaa simu kumuuliza yupo wapi?"
" vipi. Mimi nimesha fika wewe upo wapi naumevaaje"   ...."nilimuuliza nipate uhakika" .........
....." nipo mbele yako nimevaa t. Shirt jeusi" ......."jamaa lilijibu upesi nikashtuka kugeuka tu nikakutana nae"....

Itaendelea leo hiiii

Fuatia jamaa ni nani. Na anataka nini

Vipi vipimo alivyopima na kukimbia majibu


Post a Comment

 
Top