0
Wanawake wanapaswa kushauriwa kwamba njia ya kuzuia ujauzito ya matumizi ya koili ni bora zaidi kuliko njia ya dharura ya kumeza vidonge vinavyomezwa baada ya tendo la ngono (morning-afte
r pill), kwa mujibu wa ushauri mpya uliotolewa Uingereza
Limekuwa likishauriwa ni "jambo jema " kuwapatia wanawake koili kwa kipindi cha muongo.
Lakini Taasisi ya Kitaifa ya Uingereza ya afya na ubora wa Kliniki (NICE) inasema ushauri kuhusu suala hili unapaswa kuboreshwa.
Kati ya mwaka 2014 na 2015, 95% ya wanawale waliopewa vidonge vya dharura na huduma za afya na masuala ya ngono kwa ujumla walipewa vidonge vya kuzuia mimba vya... morning-after pill.
koili, ambayo pia hutambuliwa kwa lugha ya kitaalam kama...intrauterine device au IUD, ni njia inayofaa ikiwa itaingizwa katika siku tano baada ya kufanya ngono bila kinga na koili lazima zipachikwe vizuri hasa na daktari ama muuguzi aliyepewa mafunzo, katika kliniki ya afya ya uzazi ama kwenye kituo cha upasuaji.
Iwapo itakuwa vigumu kumpata daktari katika muda wa siku tano , mwanamke anaweza kushauriwa kumeza tembe za morning-after pill-kabla ya koili haijafungwa.
'Kufahamu muda ni muhimu'
Sue Burchill, mkuu wa wauguzi katika hospitali ya Brook, ambayo hutoa huduma za afya ya ngono kwa vijana 25,000 walio chini ya umri wa mika 25 kila mwaka anasema, : "tunaamini vijana wote wanapaswa kuwa na taarifa sahihi kuhusu njia tofauti za dharura za kuzuia mimba zilizopo ili wawe na uelewa kuhusu uamuzi juu ya njia iliyo bora kwa mahitaji ya binafsi, na tunatolea wito mamlaka za husika nchini kutopuuza hili kwa kupunguza udhamini kwa ajili ya huduma za afya ya ngono
"tunafahamu kwamba matumizi ya koili ndio njia iliyo inayofaa ya uzuiaji mimba wa dharura iliyopo, kwa hivyo tunapaswa kuendelea kuhakikisha tunawezesha watu kutumia injia hii na kuimarisha utaoaji wa huduma hizi miongoni mwa wale wanaozitoa."
Profesa Gillian Leng, naibu mkurugenzi mkuu wa NICE, anasema : "kwa kweli ni muhimu kwamba huduma zote za kuzuwia mimba zitolewe kwa wanawake zikiambatana na ushauri mzuri kuhusu njia za kuzuia mimba.
" Pia tunataka kuhakikisha wanawake wanaelezwa kwamba koili ni njia bora zaidi ya kuzuwia mimba kuliko tembe katika wakati wa dharura."

DK Jan Wake, wa GP na mjumbe wa shirika linalotoa maagizo kuhusu njia za kupanga uzazi, anasema : "kuelewa muda wa tendo la ngono, hata hivyo, ni muhimu na wanawake wanaoamua kutumia koili wanapaswa kutembelea kliniki walizoshauriwa kwenda mapema iwezekanavyo."

Post a Comment

 
Top