Septemba
16, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma hotuba ya kuahirisha mkutano wa
nne kwa Bunge la 11 uliodumu kwa muda wa wiki mbili, amesoma ratiba ya
serikali kuhamia Dodoma.
“Ili
kufanikisha azma ya Serikali ku
hamia Dodoma, tayari imeandaliwa ratiba
itakayowezesha Serikali kuhamia Dodoma kwa awamu, kuanzia mwezi
Septemba, 2016 hadi mwaka 2020, bila ya kuathiri bajeti yetu ya mwaka
2016/2017 kama ifuatavyo”–
1. Septemba 2016 – Februari 2017.
Waziri Mkuu na
Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wote, Manaibu Makatibu Wakuu wote
watahamia Dodoma katika Awamu ya Kwanza. Aidha, kila Wizara itatakiwa
kuhamisha Watumishi wa Idara moja au mbili, na wakati huo huo kuendelea
kuweka utaratibu wa kupeleka Watumishi wa Idara nyingine kuhamia Dodoma;
2. Machi 2017 – Agosti 2017.
Kipindi hiki
kitawapa fursa watendaji wa wizara mbalimbali kuweka katika Bajeti zao
za mwaka 2017/2018 gharama za kuendelea kuhamisha watumishi wake kuja
Dodoma.
3. Septemba 2017 – Februari 2018.
Katika awamu hii, Wizara zitaendelea na uhamishaji wa Watumishi wa Idara zilizo ndani ya Wizara.
4. Machi 2018 – Agosti 2018.
Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.
5. Septemba 2018 – Februari 2020.
Katika kipindi hiki, Wizara zinatakiwa kuendelea kuhamisha watumishi wake.
6. Machi 2020 – Juni 2020.
Katika kipindi
hiki, Ofisi ya Rais ikiongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, watakuwa wanahamia Dodoma.
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa alitumia wasaa huu kuzishauri Wizara zote kuanzisha
mifumo ya utunzaji kumbukumbu wa kielektroniki badala ya kuhama na
mafaili kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma, tunataka Dodoma iwe ya
kielektroniki, alisisitiza Waziri Mkuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment