Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kesho tarehe 12 Sep
temba, 2016
anatarajiwa kuwasili Mjini Lusaka nchini Zambia kwa ziara ya siku tatu ambapo
pamoja na mambo mengine atahudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa
Sita wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu zitakazofanyika keshokutwa
tarehe 13 Septemba, 2016 katika Jiji la Lusaka.
Rais Magufuli
anafanya ziara hii ya kwanza nchini Zambia akiwa pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya
Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Kamati
hiyo inajulikana kwa jina la SADC-Troika.
Dkt.
Magufuli alipokea kijiti cha Uenyekiti wa SADC-Troika kutoka kwa Rais wa nne
Jamhuri ya Msumbiji Mhe. Filipe Jacinto Nyusi katika Mkutano wa 36 wa SADC
uliofanyika katika Jiji la Mbabane nchini Swaziland tarehe 01 Septemba, 2016.
Katika
Ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kukutana na Viongozi mbalimbali wa nchi za
Afrika watakaohudhuria sherehe hizo zitakazofanyika katika Uwanja wa Mashujaa
Jijini Lusaka.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano, IKULU
Lusaka
11
Septemba, 2016
Related Posts
VIONGOZI WA DINI WA WASHAMBULIA CHADEMA
Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi[...]
Sep 24, 2016KWA USHUJAA HUU CHADEMA WANATAKIWA KUIGWA
September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke kimemfukuza uanachama[...]
Sep 24, 2016LIPUMBA APEWA WENYEKITI CUF
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Prof. Ibrahim Lipumba bado[...]
Sep 24, 2016CUF WAJIBU BAADA YA LIPUMBA KUTANGAZWA KUWA MWENYEKITI
Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza[...]
Sep 24, 2016NCHI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE IMEZUKA KANANGA
Ghasia za siku mbili katika mji wa Jamhuri ya kidemorasi ya Congo zimesababisha vifo vya watu 10.[...]
Sep 24, 2016BODI YA HABARI WA MWACHIA UONGOZI RAISI MAGUFURI
Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavy[...]
Sep 24, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.