Hivi karibu balozi wa korea nchini Tanzania Bw Song Geum Young akiwa na NGO ya Kutoka Korea ya World share alitembelea jimbo la mafinga mjini kwa lengo la kujionea changamoto za jimbo hilo na kutafuta njia za kutoa msaada wa kutatua baadhi ya changamoto hizo na walitoa msaada wa taa ndogo za solar kwa kaya masiki mia saba.
Baada ya balozi huyo kurudi jijini Dar es Salaam alimuagiza Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kutembelea jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti kwa kina baadhi ya changamoto za jimbo hilo ambazo alikuwa amezianisha hapo awali ili kuweza kusaidia kuzitatua.
Aidha mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee alifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za jimbo la mafinga mjini na kuzifanyia tafiti changamoto zilizopo kama uhaba wa maji na kuahidi kuzitatua kwa kuwa ameshazifanyia utafiti.
“Leo nimetembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga na nimejionea shida ya upatikanaji wa maji hivyo kwa kuwa NGO yetu inajihusisha na uchimbaji wa visima hivyo tumewasilisha taarifa hizi makao makuu ya ofisi zetu na tunasubili majibu”alisema Bw Donsun Lee.
Bw Donsun Lee alimpongeza mbunge wa jimbo mafinga mjini Cosato Chumi kwa juhudi alizozifanya za kuwashawishi kutembelea jimbo hilo na kujionea baadhi ya changamoto ambazo wanaweza kuzitatua kwa kushiriana na mbunge huyo.
Katika ziara hiyo Bw Lee na timu yake walitembelea Shule za Msingi Makalala, Mkombwe, Ndolezi na Mwongozo na Shule ya Sekondari Luganga.
Aidha baada ya tafiti hizo, Bw Lee atawasilisha taarifa zake Makao Makuu ya NGO ya Serving Friends International huko Seoul, Korea.
Nia ya kufanya tafiti hizo ni kuiweka Katika Mipango Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwa sababu ndo utaratibu wa NGO hiyo ambayo kwa Sasa wanachimba visima mkoani Singida
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la mafinga Cosato Chumi amemshukuru Mkurugenzi wa NGO ya Kutoka Korea ya Serving Friends International Bw Donsun Lee kwa kufanikisha kufanya tafiti ambazo amejine mwenye na kuleta matumaini kwa wananchi wa jimbo hilo la kutatuliwa tatizo la maji kwa kuchimbiwa visima na taasisi hiyo.
Chumi ameongeza kuwa haya ni matokeo ya ziara ya Balozi wa Korea ambaye alitembelea jimbo la Mafinga Mwezi mmoja uliopita na kujionea changamoto hizo.
Lakini mbunge Chumi amewataka wananchi wa jimbo la mafinga kufanya kazi kwa kujituma na kuunganisha na nguvu za mbunge wao ili kupata maendeleo kwa kasi inayotakiwa.
“Unakuta mbunge nahangaika kuwaletea maendeleo wananchi wangu kama hivi mnavyoona lakini ukienda vijiweni unakuta wananchi wanacheza bao,pooltable na wengi wanapiga soga zisizo na malengo,wakati wangeutumia muda huo kufanya kazi jimbo la mafinga mjini litakuwa na maendeleo ya kasi sio muda”.alisema Chumi
Related Posts
VIONGOZI WA DINI WA WASHAMBULIA CHADEMA
Viongozi wa Dini nchini, wamesema Rais JOHN MAGUFULI Hajakataa kuzungumza wala kuwapuuza viongozi[...]
Sep 24, 2016KWA USHUJAA HUU CHADEMA WANATAKIWA KUIGWA
September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke kimemfukuza uanachama[...]
Sep 24, 2016LIPUMBA APEWA WENYEKITI CUF
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema kuwa Prof. Ibrahim Lipumba bado[...]
Sep 24, 2016CUF WAJIBU BAADA YA LIPUMBA KUTANGAZWA KUWA MWENYEKITI
Baada ya kupokea Ushauri huo, The Civic United Front (CUF – Chama Cha Wananchi) kinapenda kueleza[...]
Sep 24, 2016NCHI YA KIDEMOKRASIA YA KONGO VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE IMEZUKA KANANGA
Ghasia za siku mbili katika mji wa Jamhuri ya kidemorasi ya Congo zimesababisha vifo vya watu 10.[...]
Sep 24, 2016BODI YA HABARI WA MWACHIA UONGOZI RAISI MAGUFURI
Bodi ya Uhuru Media Group inayosimamia vyombo vya habari vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambavy[...]
Sep 24, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.